Ticker

6/recent/ticker-posts

WANAWAKE WA ZIC ARUSHA, DODOMA WAKAMILISHA WIKI YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI


Picha ya pamoja ya uongozi wa Shirika la Bima la Zanzibar (ZIC) wakiwa na Katibu wa Shirika hilo Asha Rashid wakiwa katika shule ya Sekondari Arusha girls mara baada ya kukabidhi taulo za kike wakisikiliza machache kutoka Kwa wenyeji wao Katibu wa Shirika la Bima la Zanzibar (ZIC) Tawi la Arusha akimkabidhi Mwanafunzi wa shule ya Sekondari Arusha girls box la taulo za kike Mkurugenzi wa Rasilimali watu wa Shirika la Bima la Zanzibar (ZIC) Salma yusuf akizungumza na wanafunzi wa shule ya Sekondari Dodoma mara baada ya kuwatembelea na kuwapatia zawadi za taulo za Kike kama sehemu ya kuhakikisha wanafunzi hao wakike wanapata Hedhi Salama

Wanafunzi wakisikiliza Kwa makini ujumbe kutoka Kwa Mkurugenzi Rasilimali watu wa Shirika la Bima la Zanzibar (ZIC) Salma Yusuf mara baada ya kuwasili katika shule ya sekondari ya Dodoma Kwa ajili ya kutoa taulo za kike ikiwa ni sehemu ya Kuadhimisha Siku ya Wanawake Dunia na kuhakikisha Mabinti hao wanapata Hedhi Salama

*********************

KAMPENI ya ugawaji wa taulo za kike Kwa baadhi ya shule kutoka Shirika la Bima Zanzibar (ZIC) lahitimishwa rasmi katika wiki ya Kuadhimisha Siku ya Wanawake Dunia Jijini Dodoma.

Kwa upande wake pia Mkurugenzi wa Rasilimali watu wa Shirika hilo Salma yusuf wametembelea shule ya Sekondari Dodoma na kukamilsha wiki ya Siku ya Wanawake Dunia Kwa kuendelea kutoa zawadi za taulo za kike Kwa Mabinti ikiwa ni ishara ya kuhakikisha Shirika hilo linajali usalama wa Afya za wanafunzi Mashuleni kama wanavyowakikishia wateja wao usalama wa bima zao.

"Tunakamilsha wiki hii ya "Siku ya Wanawake Duniani Kwa kuungana na Nyie na kuwapa zawadi ambazo zitasaidia Kwa muda mchache Ili Kuwahakikishia usalama mnapokuwa kwenye siku zenu ,hivyo Shirika limeichagua shuleni yenu kuwapatia zawadi hizo."

Hata hivyo kwa upande wake Muwakilishi kutoka Shule ya Sekondari Dodoma ametoa pongezi kwa uongozi mzima wa Shirika hilo na kuwaomba zoezi hilo la zawadi hizo ziwe mara Kwa mara kwani uhitaji ni wa Kila siku.

Katibu Wa Shirika la Bima la Zanzibar Asha Rashid alikabidhi taulo za Kike kwa shule ya Sekondari ya Arusha girl amesema Kutokana na kuwepo uhitaji wa taulo hizo hususani Mabinti wanapokua shuleni Shirika hilo limewiwa kutoa zawadi hizo Kwa wanafunzi hao.

Hata hivyo mbali na kutoa zawadi hizo Katibu aliwapa Elimu Mabinti hao kuhusu Hedhi Salama pamoja na kuvunja upendeleo Ili kuleta Mabadiliko (Bias) katika Taifa letu.

Post a Comment

0 Comments