*******************
Na. Dominic Haule
Wafanyabiashara wa Ndani ya nchi wametakiwa kuendelea kukuza ushirikiano na Wafanyabiashara wengine kutoka nje ya nchi ikiwemo wafanyabiashara kutoka n nchi ya Uturuki ili kuhakikisha Wanakuza na kuongeza thamani ya Mnyoro wa Uchumi wa nchi.
Wito huo Umetolewa na Ndugu.Paul koyi Rais wa chemba ya Biashara Viwanda na kilimo(TCCIA) Wakati wa Mkutano wa siku moja wa Wafanyabiashara na wekezezaji zaidi 25 kutoka nchini Uturuki na wandani ya nchi ikiwa lengo Kubadilishana uzoefu na kupeana Fursa za Uwekezaji pande hizo mbili.
Ndugu Koyi Amesema kuwa lengo la serikali nikuhakisha Wana wapa Fursa Wafanyabiashara na wawekezaji wa Ndani ya nchi kutafuta masoko na kuwekeza nje ya nje ikiwa lengo kukuza Ushirikiano katika Uwekezaji.
Hata hivyo amesema kuwa Miongoni mwa mwa vitu wanavyo peleka nchini Uturuki ni Malighafi ya mazao hivyo basi wanaomba Wafanyabiashara kupeleka nchini humo kwa wingi na kuongeza ongezekao la thamani ikiwa lengo ni kuchochea Uchumi wa nchi na wakulima kwa Ujumla ili wanufaike na kilimo.
Wakati huo huo Amesema kuwa Miongoni mwa makampuni yalio kuja nchini kushiriki kutoka nchini Uturuki ni ya Umeme hivyo wamekutana na Wafanyabiashara Biashara wa Ndani wanaofanya Biashara ya vifaa vya Umeme hapa Tanzania ili wapeane Fursa za Uwekezaji.
Naye Mwenyewekiti wa Taasisi ya Sekta Binafs TPSF Bi.Angelina Ngalula amesema kuwa Biashara ya nchi ya Utuluki na Serikali ya Tanzania imeendelea kukua na kufikia kipindi Cha Mwaka Mmoja Dora Milioni Mia Tatu tofauti na Zamani ilikuwa Dora Milioni Miambili na Hamsini Ndani ya Kipindi Cha Mwaka Mmoja imekua zaidi hivyo Kupitia juhudi Rais Jamhuli ya Muungano Wa Tanzania Mh Samia Suluhu Hassani .
Aidha Bi. Ngalula amesema kuwa Utuluki Ina mpango wa kujenga Vituo vyao hapa Tanzania vya kuweza kuonesha Fursa ambazo zinapatoka nchini Uturuki kwa kushirikiana na Watanzania ili kuhakikisha wanachochoea Uchumi wa nchi hasa katika kuwainua Watanzania.
Mkutano huo ulifanyika Jijini Dar es salaam na Kushiri Wafanyabiashara na Wawekezaji Tofauti katoka Ndani nchi na nchi ya Utuluki ulio andaliwa na nchi Uturuki Chini ya Balozi wa nchi hiyo Balozi wa Uturuki nchini Tanzania Dk,Mehment Gulluoglu kwa Kushirikiana na Serikali ya Tanzania
0 Comments