Mkurugenzi WWF Dkt Amani Ngusalo akikabidhi jezi kwa Wanafunzi wa vyuo kulia kwake Mwakilishi wa TFF Aly Ruvu.
Mkurugenzi Dkt Amani Ngusalo akizungumza.
************
Na Magrethy Katengu, Dar es salaam
Licha ya jitihada mbalimbali zinazofanywa za kulinda mazingira bado kuna uharibifu wa mazingira ambapo takwimu zinaonyesha kuwa zaidi ya hekta 460 za misitu kila mwaka hupotea kutokana na shughuli za kibinadamu.
Ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Shirika la Word Wildlife Fund(WWF) Dkt. Amani Ngusalo katika hafla ya kuadhimisha wiki ya kampeni ya upandaji miti itakayohitimishwa Machi 27 ambayo ni siku ya Earth hour Duniani ambapo kutakuwa ba shughuli mbalimbali ikiwemo ligi ya mpira wa miguu pamoja na upandaji miti katika maeneo mbalimbali ikiwemo Ifakara,Kilombero,Dodoma,Pwani ,Dar es salaam
Aiadha amesema kuwa ligi hiyo itahusisha vyuo vikuu 8 ikiwemo UDSM, TUDARCO na NIT pamoja kampeni ya kupanda miti 10000 katika maeneo mbalimbali ya Tanzania na kuhamasisha watu kuendelea kutunza mazingira ili kuondokana na athari ya mabadiliko ya tabia nchi inayosababisha ukame,mafuriko
Hata hivyo amesema Shirika la World Wildlife Fund (WWF) watashirikiana na Wizira ya Maliasili na Utalii pamoja na ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira katika kuhakikisha kuwa lengo la uhifadhi wa mazingira na upandaji miti linafanikiwa katika ili lengo lililopangwa linafikiwa.
“Kesho tutaanza kampeni ya upandaji miti Dar es Salaam, Pwani na Chato ikiwa ni kumbukizi ya kifo cha Rais wa Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli pamoja na kuanza kwa ligi ya mpira wa miguu itakayo simamiwa na shirikisho la mpira wa miguu (TFF)” Amesema Dkt. Ngusalo.
Kwa upande wake Mwakilishi wa TFF Ally Ruvu amewataka washiriki wa mashindano hayo kuhakikisha kuwa wanafuata taratibu zinazotakiwa ikiwe sheria 17 za mpira wa miguu pamoja na konyesha vipaji vyao kwani soka ni ajira.
“Niwakumbushe vijana hususani watakaoshiriki ligi hii kutambua kuwa mpira ni ajira na kupitia michezo hiyo TFF itachambua wenye vipaji zaidi ili wakacheze katika timu ya taifa ya vijana “ Amesema Ally Ruvu.
0 Comments