Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akizungumza na watumishi wa Wakala wa Vipimo (WMA) mara baada ya kutembelea banda lao leo kwenye Maonesho ya Pili ya Bidhaa za Wanawake Wajasiriamali katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kutembelea banda la Wakala wa Vipimo (WMA) kwenye Maonesho ya Pili ya Bidhaa za Wanawake Wajasiriamali katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akizungumza jambo na Afisa Mtendaji Mkuu Wakala wa Vipimo (WMA) Bi. Stella Kahwa mara baada ya kutembelea banda la Wakala wa Vipimo (WMA) kwenye Maonesho ya Pili ya Bidhaa za Wanawake Wajasiriamali katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam .
**********************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo amewapongeza Wakala wa Vipimo (WMA) kwa kuendelea kutoa elimu ya Vipimo kwa Wajasiriamali kwenye Maonesho ya Pili ya Bidhaa za Wanawake Wajasiriamali yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza mara baada ya kutembelea banda la WMA kwenye viwanja hivyo Waziri Jafo amesema uwepo wa Wakala hao katika maonesho hayo kutawarahisisha wajasiriamali wanawake kupata fursa ya kuelimishwa kuhusu vipimo.
Amesema suala la vipimo ni muhimu hasa katika masuala ya biashara, hivyo kupitia maonesho hayo yatawajengea uelewa mkubwa wajasiriamali namna watakavyotumia vipimo kwenye biashara zao.
Nae Afisa Mtendaji Mkuu Wakala wa Vipimo (WMA) Bi. Stella Kahwa amesema wameshiriki katika maonesho hayo kwaajili ya kutoa elimu ili wafungashe kwa usahihi bidhaa zao na kuweza kushindana kwa masoko ya ndani na nje.
"Bila ufungishaji uliosahihi na kutumia vipimo vilivyosahihi inamaana unaweza usifungashe bidhaa zako kwa usahihi unaotakiwa".Amesema Bi.Stella.
Amesema ukilinganisha maonesho ya mwaka huu na maonesho ya mwaka, kuna mabadiliko makubwa kwasasa wajasiriamali bidhaa zao wanafungasha kwa usahihi licha ya kuwepo kwa makosa madogo madogo ambayo yanaweza kurekebishika .
0 Comments