Ticker

6/recent/ticker-posts

YANGA SC YASHEREHEKEA MWAKA MMOJA WA RAIS SAMIA MADARAKANI KWA KUONDOKA NA USHINDI WA 2-0 DHIDI YA KMC
**********

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

YANGA yazidi kujiweka pazuri katika kuutafuta Ubingwa wa NBC Premier League ambapo leo hii imeendeleza ushindi katika ligi hiyo baada ya kuifunga KMC mabao 2-0.

Yanga ilianza kupata bao la kwanza kupitia kwa Djuma Shabani akifunga bao la kichwa akipokea mpira uliopigwa kona na Chiko Ushindi na kuwafanya waongoze katika kioindi cha kwanza.

Fiston Mayele hakuwa na bahati ya kupachika bao leo japokuwa aliweza kusababisha bao ambalo alijifunga Adrew Vicent .

Yanga inaendelea na wimbi la ushindi pasipo kuruhusu bao kufungwa kwa michezo mingi mfululizo.

Kabla ya mechi kuanza kulikuwa na burudani kwa mechi kati ya Viongozi wa Yanga na Wasanii wa bongo freva na bongo muvi na baadae kulipigwa burudani ya Muziki kama maadhimisho ya mwaka mmoja akiwa madarakani Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu

Post a Comment

0 Comments