Ticker

6/recent/ticker-posts

MALIMA AKERWA KUTOKAMILIKA KWA TAARIFA ZA MAOFISA LISHE NGAZI ZA HALMASHAURI ZA WILAYA 11


***********************


Na Hamida Kamchalla, Tanga.

Mkuu wa Mkoa wa Tanga Adam Malima ameonesha kutoridhishwa na taarifa ya hali ya lishe Mkoa huo kutokana na kutokamilika kwa taarifa za Maofisa lishe katika ngazi za halmashauri za Wilaya 11 zilizopo mkoani humo.

Akiendesha kikao hicho jana, Malima alisema kuna ukakasi katika taarifa zilizoandaliwa baina ya Wakurugenzi na Wakuu wa Wilaya kutokana na kutopitia taarifa zao katika vikao wanavyopaswa kukaa kwenye halmashauri zao.

Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Basila Mwanukuzi alibainisha kwamba ili kuendelea kujaza mikataba mipya ya huduma ya lishe wanahitaji kushiriki kikamilifu na kusikia utekelezaji katika vikao vinavyokaliwa ngazi ya halmashauri.

"Kitakachotufanya sisi wakuu wa Wilaya tujaze miataba upya hatuhitaji maelezo, bali tunahitaji yale tuliyokubaliana kwamba, kuhakikisha halmashauri lazima ifanye vikao, na mimi nikiwa DC sijapata taarifa ya kufanyika kwa kikao hicho" alisema Mwanukuzi.

Hata hivyo Malima aliwataka viongozi hao kuzingatia miongozo wanayopewa kwani hali hiyo inaonesha kwamba kuna upuuziaji wa maagizo kwa baadhi yao huku akiahirisha kikao hicho na kutoa akitoa wiki moja akiwataka wakakae upya na kupitia taarifa zao.

"Mnapoona miongozo msiipuuzie, siku litakuja kubumburuka huko halafu sijui mtaanzia wapi, tukubaliane kwamba tutafanya hiki kikao baada ya wakuu wa Wilaya kupitia taarifa zao, mkakae vikao vyenu kwa kufuata kanuni na taratibu" alisema.

"Siku ya jumatano, tarehe 13 mwezi huu, wiki moja kuanzia sasa kila mmoja wenu aje na taarifa yake, nendeni mkafanye viiao vya tathmini na ushirishwaji" alisisitiza miuu huyo.

Post a Comment

0 Comments