Ticker

6/recent/ticker-posts

PSSSF YATWAA TUZO KILELE CHA SIKU YA AFYA NA USALAMA MAHALI PA KAZI

NA MWANDISHI WETU, DODOMA


MFUKO wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) umepewa Tuzo ya Kutoa Huduma Rafiki kwa Wazee na Wagonjwa wakati wa Maonesho ya Siku ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi Duniani iliyofikia kilele leo Aprili 28, 2022 kwenye viwanja vya Kituo cha Mikutano Jakaya Kikwete jijini Dodoma.

Aliyekabidhi Tuzo hiyo ni Mgeni Rasmi katika sherehe hizo Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Lazaro Ndalichako na ilipokelewa na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, PSSSF, Paul Kijazi.

Siku ya usalama na afya mahali pa kazi Duniani ni siku ya Kimataifa ya kufanya kampeni ya kuboresha usalama na afya ya wafanyakazi, lengo ni kuondoa hali zote hatarishi mahali pa kazi na hivyo kuifanya kazi iwe ya hadhi na heshima na hufanyika kila mwaka kuelekea Siku ya Wafanyakazi Duniani yaani Mei Mosi.

Kwa mujibu wa Afisa Uhusiano Mkuu wa PSSSF, Abdul Njaidi alisema ushiriki wa Mfuko kwenye maonesho hayo ilikuwa ni fursa nzuri ya kukutana na wanachama pamoja na wananchi kwa ujumla ambao walifaidika kwa kupata elimu kuhusu shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na Mfuko.

Alisema wote waliofika kwenye banda la PSSSF walikutana na wahudumu wa Mfuko ambao kazi yao kubwa ikiwa ni pamoja na kuwapokea wageni kwa bashasha na kutoa elimu kuhusu Mafao yatolewayo na Mfuko, namna ya kupata taarifa za michango kwa njia ya mtandao, jinsi ya mwanachama kuhakiki taarifa zake

“Majukumu ya msingi ya Mfuko ni pamoja na Kuandikisha Wanachama, Kukusanya Michango, Kulipa Mafao lakini pia Kuwekeza kwa njia ya hisa kwenye mabenki na kwenye maeneo mengine kwa mujibu wa sharia” alisema na kuongeza……….Safari hii tumeshirikiana na Kampuni yetu tanzu ya Kilimanjaro International Leather Industries Co. Limited (KLICL) inayojisughulisha na utengenezaji wa bidhaa za ngozi kama vile viatu, mikanda na mapochi.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu ((Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Prof. Joyce Lazaro Ndalichako (wapili kushoto), akimkabidhi tuzo ya Kutoa Huduma Rafiki kwa Wazee na Wagonjwa wakati wa Maonesho ya Siku ya Usalama na Afya Mahali pa kazi, Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma, (PSSSF), Bw. Paul Kijazi wakati wa Maonesho ya Siku ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi Duniani iliyofikia kilele leo Aprili 28, 2022 kwenye viwanja vya Kituo cha Mikutano Jakaya Kikwete jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa TUCTA Bw. Henry Mgunda (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na waanyakazi wa PSSSF kwenye banda la Mfuko huo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu ((Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Prof. Joyce Lazaro Ndalichako (wapili kulia mstari wa mbele), Naibu Waziri Mhe. Ummy Nderiananga (wanne kulia) wakiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi na wafanyakazi wa PSSSF
Afisa Uhusiano Mkuu, PSSSF, Bw. Abdul Njaidi (kushoto) akimuangalia Msanii maarufu nchini Mrisho Mpoto wakati akijipima kiatu cha kampuni ya KLICL kinachomilikiwa kwa ubia kati ya PSSSF na Magereza alipotembelea kwenye banda la Mfuko huo.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu PSSSF, Bw. Ansigar Mushi (katikati) akimuhudumia mwananchi huyu kulia aliyetembelea banda la PSSSF.

Post a Comment

0 Comments