Ticker

6/recent/ticker-posts

WAZIRI MAKAMBA -WATANZANIA MSITAHARUKI HAKUNA UHABA WA MAFUTA NCHINI


Waziri wa Nishati Mhe. Januari Makamba akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukutana na Wadau waagizaji na wafanyabiashara, wa mafuta nchini katika Ofisi ndogo iliyopo Jijini Dar es Salaam.


*****************************


Na Magrethy Katengu-Dar es salaam


Serikali kupitia Wizara ya Nishati imesema hakuna uhaba wa mafuta nchini hivyo wananchi wasiwe na taharuki yeyote kwani mafuta yaliyopo kwenye maghala,bandarini,na vituoni yanatosheleza kwa kipindi cha muda mrefu.


Akizungumza leo Aprili 6,2022 Jijini Dar es Salaam Waziri wa nishati Mhe.Januari Makamba katika kikao kilichowakutanisha waagizaji,wasambazaji na wauzaji wa Mafuta nchini kujadiliana hali halisi ya mwenendo wa biashara ya Mafuta na ustawi ambapo amesema kuna taharuki imejitokeza miongoni mwa wananchi hivyo hofu ya kuwa kuna uhaba mafuta siyo kweli.


Amesema mafuta ya petroli yapo Lita za ujazo Milioni 119 ambazo zinatosheleza kwa siku 27 na ,Mafuta ya dizeli Lita za ujazo Milioni 116 yanatosheleza kwa siku 19 mengine yanaendelea kuja, mafuta ya taa lita Milioni 6 yanajitosheleza kwa siku 120 ,Mafuta ya ndege lita za ujazo Milioni 12 yanatosheleza kwa siku 35.


"Kuna meli zimewasili Nchini na zinaendelea kushusha mafuta ya ikiwemo dizeli ambapo ukichanganya kiwango kilichopo na kinachoendelea kushushwa kinafanya kutosheleza takribani siku thelathini tatu petroli nayo iliyopo na inayoendelea kushushwa kutosheleza kwa siku thelathini na saba na hivyo tuna mafuta mengi ya kutosha "alisema Waziri Makamba nyingine


Pia Waziri Makamba amesema mafuta yataendelea kuuzwa kwenye vituo na kwa utaratibu wa kawaida hivyo hakuna haja ya kupaniki Wala kukimbilia kujaza matenki majumbani uendelee utaratibu wa kawaida siyo kujazana hofu na taharuki


Hata hivyo amesema mafuta yanayotakiwa kutumika mwezi wa tano na wa sita tayari yameshaagizwa hivyo kwa sasa utaratibu unaendelea kukusanywa mahitaji kwa ajili ya kuagiza mafuta ya mwezi wa saba serikali kwa kushirikiana na wadau wa biashara wanaendekea kuhakikisha kusitokee uhaba kabisa


"Niseme suala la bei ya mafuta imepanda kuanzia Jana ilitangazwa Jambo ambalo halikwepeki kutokana na mwenendo na mwezi ujao zitapanda ni za hakika Nchi nyingi zinaagiza mafuta kwa nchi zinazozalishwa mafuta na hii bidhaa inauzwa kwenye soko la Dunia na mwenendo wa bei zinafuta soko la Dunia kunapokua na mahitaji bei inapanda kunapokua na upatikanaji mwengi bei zinashuka hivyo mwenendo wa shughuli za kiuchumi na kisiasa unaathiri upatikanaji "alisema Waziri Makamba


Hata hivyo amesema kuanzia disemba 2019 hadi 2021 Dunia ilikumbwa na janga la ugonjwa wa Covidi-19 Nchi nyingi zilijifungia hakuna usafiri wa ndege,magari kwenda nchi jirani hivyo kulikua hakuna uhitaji na mafuta yalikua mengi na bei ya mafuta katika soko la Dunia ilishuka hadi kufikia sifuri watu waliokua wanafanyia biashara ni wenye matenki na wazalishaji walisimama kwa kukosa biashara baada ya Covid-19 kupungua na watu kurudi katika shughuli zao kwa kufunguka viwanda,ndege kuanza kuruka hivyo kufunguka biashara Duniani kukaleta uhitaji mkubwa wa mafuta kasi ya uzaliji ikawa ndogo hivyo kupelekea ongezeko la bei


Sanjari na hayo kuanza kwa Vita ya Ukraini na Urusi na Nchi kwani Ukraini ni wazalishaji wa mafuta nayo imechangia kupanda kwa bei hivyo kutokana na matukio mawili yaliyotokea Duniani haujawahi kutokea kupanda kwa bei hadi kufikia asilimia miamoja hata hivyo serikali iko makini kuhakikisha yapo na yanapatikana


Kwa upande wake Mwenyekiti wa chama Cha waagizaji Mafuta Nchini Oladrod Costa amesema hakuna uhaba wa Mafuta kuna Mafuta ya kutosha kwenye matenki kwani kuna meli zinasubiria kushusha nyingine ziko njiani bezetu ni zuri kwa watanzania waondoekane na hofu

Post a Comment

0 Comments