Ticker

6/recent/ticker-posts

BALOZI SOKOINE AKUTANA NA BALOZI WA ANGOLA NCHINI

Balozi wa Angola nchini Mhe. Sandro de Oliveira (katikati) akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili katika Ofisi za Wizara jijini Dodoma kulia ni mwenyeji wake Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Joseph Sokoine
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Joseph Sokoine akiangalia nyaraka wakati alipokutana na Balozi wa Angola nchini Mhe. Sandro de Oliveira katika Ofisi za Wizara jijini Dodoma
Balozi wa Angola nchni Mhe. Sandro de Oliveira akizungumza wakati alipokutana na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Joseph Sokoine katika ofisi za Wizara jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Joseph Sokoine (kulia) akizungumza na Balozi wa Angola nchini Mhe. Sandro de Oliveira (kushoto) walipokutana katika Ofisi za Wizara jijii Dodoma


*********************

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Joseph Sokoine amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Angola nchini Mhe. Sandro de Oliveira katika Ofisi za Wizara jijini Dodoma.

Akizungumza katika kikao hicho Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Joseph Sokoine amemuhakikishia Mhe. Balozi Sandro de Oliveira utayari wa Tanzania katika kuendelea kushirikiana na Angola katika kukuza na kuimarisha uhusiano baina ya nchi hizo.

"Mhe. Balozi, nikuhakikishie kwamba Tanzania itaendelea kushirikiana na Angola ili kuimarisha na kukuza uhusiano kati ya Tanzania na Angola na kuongeza kuwa Tanzania inadhamiria kuufikisha uhusiano huo mbali zaidi,’’ alisema Balozi Sokoine.

Naye Balozi Sandro amemshukuru Balozi Sokoine kwa mazungumzo yao na kuahidi kwamba Angola itaendelea kushirikiana na Tanzania ili kuendelea kuulinda uhusiano ambao uliasisiwa na viongozi wa mataifa hayo.

Viongozi hao wamekubaliana kuendela kuimarisha uhusiano wa karibu na wa kindugu uliopo kati ya Tanzania na Angola ambao umekuwepo kwa miaka mingi ulioasisiwa na waasisi wa mataifa hayo Hayati Mwalimu Julius Nyerere na Hayati Antonio Agustino Neto ikiwa ni pamoja na Tanzania kukisaidia Chama cha MPLA cha Angola kupigania uhuru wa nchi hiyo.

Viongozi hao pia wamekubaliana kuendelea kushirikiana katika sekta mbalimbali za kidiplomasi, kiuchumi, kisiasa na kijamii ikiwa ni pamoja na kufanya kazi kwa pamoja na kushughulikia changamoto zinazojitokeza katika sekta mbalimbali ili kuchochea ukuaji wa uchumi baina ya nchi

Post a Comment

0 Comments