Ticker

6/recent/ticker-posts

KATIBU MAGANGA AWAPA KONGOLE HOSPITALI YA BENJAMIN MKAPA


Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga (wa pili kushoto) akiwa katika ziara ya kutembelea na kukagua mabwawa ya kutibu majitaka katika eneo la Hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Mazingira leo tarehe 29 Mei, 2022.Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga akipanda mti katika eneo la mabwawa ya kutibu majitaka katika eneo la Hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Mazingira leo tarehe 29 Mei, 2022. Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga akipata maelezo kuhusu mabwawa ya majitaka kutoka kwa Meneja wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mhandisi Aron Joseph wakati wa ziara ya kutembelea na kukagua mabwawa ya kutibu majitaka katika eneo la Hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Mazingira leo tarehe 29 Mei, 2022.

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga (wa tatu kushoto) akipata maelezo kuhusu ufanyaji kazi wa tanuru la kuchomea taka kilichopo Hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma kutoka kwa Afisa Mazingira Bw. Manara Donald wakati wa ziara ya kikazi hospitalini hapo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Mazingira leo tarehe 29 Mei, 2022 Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga akizungumza na wataalamu wa mazingira na waandishi wa habari mara baada ya ziara ya kikazi katika Hospitali ya Benjamin Mkapa na mabwawa ya kutibu majitaka jijini Dodoma wakati wa ziara ya kikazi ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Mazingira leo tarehe 29 Mei, 2022. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu (Muungano) Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Abdallah Hassan Mitawi na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Seif Shekalaghe.

****************

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga ametoa pongezi kwa Uongozi wa Hospitali ya Benjamin Mkapa Dodoma kwa kutekeleza ajenda ya Mazingira kwa vitendo.

Bi. Maganga ametoa pongezi hizo leo tarehe 29 Mei, 2022 mara baada ya kufanya ziara ya kkazi katika Hospitali ya Benjamin Mpaka kwa lengo la kujionea jitihada za wadau katika upandaji wa miti na usafi wa Mazingira.

Akiwa Hospitalini hapo Bi. Maganga amejionea matumizi ya nishati mbadala wa kuni na mkaa kwa matumizi ya kupikia na kutoa rai kwa taasisi zingine kuiga mfano huo ili kupunguza kiasi cha ukataji wa miti kwa matumizi ya kuni na mkaa.

"Tumeshuhudia hapa, matumizi ya gesi kama nishati ya kupikia, nawapongeza sana, ninyi ni mfano wa kuigwa," alisisitiza Bi. Maganga.

Pia, Bi. Maganga ameuagiza uongozi wa Hospitali ya Benjamin Mkapa kuhakikisha kuwa eneo lililotengwa na kutumika kwa ajili ya kutibu majitaka halivamiwi na kutumika kwa matumizi mengine.

"Eneo hili lihifadhiwe vizuri kusiwe na shughuli nyingine za kijamii," alisema Bi. Maganga.

Katika hatua nyingine wakati akitembelea na kukagua mabwawa ya kutibu majitaka, Katibu Mkuu huyo aliipongeza Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) kwa kusimamia vyema mradi huo.

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Seif Shekalaghe amesema Wizara ya Afya ina Taasisi nyingi na Hospitali ya Benjamin Mkapa ni moja ya Taasisi za mfano wa kuigwa.

Katika kuadhimisha Siku ya Mazingira shughuli mbalimbali za hifadhi na usafi wa mazingira zinafanyika katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dodoma zikihusisha wananchi, taasisi, shule, vyuo na viongozi mbalimbali.

Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani yatafikia kilele chake tarehe 5 Juni, 2022, Katika Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete, ambapo Mgeni Rasmi ni Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Post a Comment

0 Comments