Ticker

6/recent/ticker-posts

MAABARA YA UFUATILIAJI VINA SABA VYA UGONJWA WA MALARIA YAZINDULIWA LEO JIJINI DAR ES SALAAM


Mganga Mkuu wa Serikali Dkt.Aifello Sichalwe akikata utepe wa kuzindua maabara ya ufuatiliaji vina Saba vya malaria.
Mganga mkuu wa serikali Dkt.Aifello Sichalwe akozungumza katika hafla ya uzinduzi wa maabara ya kufuatilia vinasaba vya ugonjwa wa Malaria.

Mganga Mkuu wa serikali Dkt Aifello Sichalwe akikagua maabara hiyo.

************

Na Magrethy Katengu

Serikali kupitia Taasisi yake ya Utafiti wa Magonjwa ya binadamu (NIMR)imesema itahakikisha inaongeza jitihada za kutokomeza ugonjwa wa malaria ambao umekuwa tishio na kusababisha vifo vya watu wengi kila siku

Akizungumza leo Jijini Dar es salaam katika hafla ya uzinduzi wa maabara ya kufuatilia vinasaba vya ugonjwa wa Malaria, Mganga Mkuu wa Serikali Dkt.Aifello Sichalwe amesema kwamba maabara hiyo ni moja ya mkakati wa Wizara ya Afya kupitia mpango wa kudhibiti malaria kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa( TAMISEMI).

Hata hivyo amesema kuwa Mradi huo wa maabara ya ufuatiliaji wa vinasaba vya malaria una lengo la kupata ushahidi wa kina juu ya chanzo kinachosababisha ugonjwa wa Malaria nakwamba utasaidia wataalamu wa masuala ya tafiti kupata suluhisho namna ya kukabiliana na ugonjwa huo.

"Utafiti huu wa vinasaba vya malaria niwa awamu ya kwanza kutekelezwa hapa Nchini ,na unafadhiliwa na wadau wetu wa maendeleo ikiwemo umoja wa Ulaya(UN) na tunawaomba waendelee kufadhili ,pia tunaendelea kufanya mazungumzo na wadau wengine waweze kufadhili ile uwe endelevu nakufikia lengo tulilokusudia" amesema Dkt.Sichalwe.

Sanjari na hayo Dkt Sichalwe ameendelea kufafanua kwamba utafiti huo utasaidia kuwajengea uwezo NIMR Kwa kuzalisha takwimu za vinasaba vya Maleria hapa Nchini nakuzichakata kisha wizara ya afya itazitumia kufanya maamuzi ikiwemo kuandaa miongozo,kutunga sera nakutekeleza mikakati mbalimbali yakupambana na malaria huku wakiwa na ushahidi wa kisayansi.

Awali makamu mwenyekiti wa baraza la taasisi ya utafiti wa magonjwa ya binadamu( NIMR) Dr.Khadij Malima amesema kwamba utafiti wa vinasaba vya ugonjwa wa malaria utekelezaji wake umeanza tangu Mwezi Mei 2020 na inatarajiwa kukamilika mwezi oktoba 2023 ambapo kwa sasa umeanza katika mikoa kumi na tatu Nchini kote.

Amebainisha mkoa hiyo kuwa ni pamoja Dar es salaam,Morogoro,Dodoma,Manyara,Pwani,Songwe,Ruvuma,Tabora,Tanga,Kagera,Mtwara,Kigoma,Mara.

Aidha maabara imeshakamikika na inaenda kufanya kazi iliyokusudiwa ili kusaidia kuleta suluhisho la ugonjwa huo ambao umekuwa ukipoteza idadi kubwa ya watu.

Post a Comment

0 Comments