Ticker

6/recent/ticker-posts

MAKAMU WA RAIS DKT.MPANGO AFUNGUA MKUTANO WA SAYANSI WA NIMR



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akizungumza na washiriki wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 31 wa pamoja wa Sayansi ulioandaliwa na Taasisi ya Taifa ya utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) unaofanyika katika kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere Jijini Dar es salaam.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akitoa tuzo za Sayansi kwa washindi mbalimbali wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 31 wa pamoja wa Sayansi ulioandaliwa na Taasisi ya Taifa ya utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) unaofanyika katika kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere Jijini Dar es salaam.

………………………………………

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango leo tarehe 17 Mei 2022 amefungua mkutano wa 31 wa pamoja wa Sayansi ulioandaliwa na Taasisi ya Taifa ya utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) unaofanyika katika kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere Jijini Dar es salaam. Mkutano huo unashirikisha wataalamu na wadau mbalimbali wa sekta ya afya kutoka maeneo mbalimbali ndani na nje ya Tanzania.

Akizungumza na washiriki wa mkutano huo Amesema Tanzania inaunga mkono na kuamini katika ufanyaji wa tafiti zitakazokabiliana na changamoto za maradhi hapa nchini. Ameongeza kwamba mkutano huo ni fursa ya aina yake kwa wanasayansi wa Tanzania kujifunza kutoka kwa kila mmoja na kuunganisha werevu na uwezo katika kupata masuluhisho ya kimsingi kwa changamoto kuu za kiafya hapa nchini.

Makamu wa Rais amesema mkutano huo una umuhimu mkubwa kutokana na kufanyika katika kipindi ambacho dunia, Tanzania ikiwemo inapitia katika changamoto mbalimbali za magonjwa kama vile Uviko 19 pamoja na magonjwa yasioambukiza. Aidha ameongeza kwamba serikali imedhamiria kufikisha huduma za kiafya katika maeneo yote hapa nchini na itaendelea kushirikiana na wadau wote wakiwemo watafiti na sekta binafsi.

Halikadhalika Makamu wa Rais ameiagiza Taasisi ya Taifa ya utafiti wa magonjwa ya binadamu (NIMR) kuongeza kasi ya ufanyaji utafiti pamoja na kuzalisha chanjo na dawa bora za asili.

Kwa upande wake Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema wizara itaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa Taasisi ya Taifa ya utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) ili kuweza kutumiza majukumu yao kwa ufanisi. Amesema tayari NIMR imeshiriki katika tafiti mbalimbali zinazowezesha katika utungaji wa sera na mipango katika wizara ya afya ikiwemo kuwezesha Wizara kupata uhalisia wa utoaji wa chanjo ya HPV ambayo inakinga wasichana dhidi ya saratani ya mlango wa kizazi.

Nae Mkurugenzi wa Taasisi ya Magonjwa ya Binadamu (NIMR) Prof.Yunus Mgaya amemuhakikishia Makamu wa Rais Dkt..Philip Mpango pamoja na Waziri wa afya kuwa utafiti wa chanjo ya Ugonjwa wa UVIKO 19 unaendelea kufanyiwa tafiti na majibu ya utafiti huo yatakamilika mwishoni mwa mwaka huu.

Sanjari na hayo amesema kuanzia mwezi Disemba walianza kufanya tafiti ya chanjo za Corona ,kuna dozi za kutosha za chanjo ya corona kilichobaki nikuwandikisha wananchi kwenye vituo vya Dar es salaam na Mbeya ,hivyo wanafanya tafiti hizi Kwa awamu,watatoa majibu ya tafiti mwisho wa mwaka huu

Post a Comment

0 Comments