Ticker

6/recent/ticker-posts

MALIMA ATOA WIKI TATU KUKAMILIKA UJENZI WA SHULE KIJIJI CHA MSOMELA


Mkuu wa Mkoa wa Tanga Adam Malima akizungumza wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa miundombinu ya shule ya msingi na sekondari katika kijiji cha Msomela juzi wilayani Handeni.

**************

Na Hamida Kamchalla, Handeni.

MKUU wa Mkoa wa Tanga Adam Malima amesema hakuridhishwa na maendeleo ya ujenzi hivyo ametoa wiki tatu kwa halmashauri ya Wilaya ya Handeni kuhakikisha wanakamilisha ujenzi wa shule mbili katika eneo la Msomela ambazo zitatumiwa na wananchi wanaohamia kutoka Ngorongoro.


Malima alitoa agizo hilo amelitoa juzi wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa miundombinu ya shule ya msingi na sekondari katika kijiji cha Msomela wilayani Handeni.


Aidha alisema kuwa mpaka sasa hajaridhishwa na kasi ya ujenzi wa miundombinu inavyoendelea kwa sasa hali ambayo inampa wasiwasi kama wataweza kukamilisha Kwa wakati.


"Sitaki kusikia kisingizio cha hali ya hewa wala mvua wekeni mazingira ya kufanyakazi usiku na mchana Ili majengo haya yaweze kukamilika kwa wakati" alisema Malima.


Mkuu huyo alisema kuwa baada ya muda huo hataweza kuvumilia sababu zozote bali atahakikisha anachukuwa hatua stahiki kwa wale wote waliochangia kuhujumu miradi hiyo.


"Acheni mambo ya kufikiria kupata faida kwenye miradi hii kwani miradi ya Msomela ina macho ya wengi hivyo hakikisheni mnaitekeleza kwa viwango na inakamilika kwa wakati" alisisitiza Mkuu wa mkoa


Awali akisoma taarifa ya mradi huo, ofisa elimu msingi halmashauri ya Wilaya ya Handeni Nyoka alisema kuwa TAMISEMI iliweza kuwapatia kiasi cha sh milioni 400 kwa àjili ya hatua za awali za ujenzi wa majengo ya shule ya msingi na sekondari.


Aidha alisema kwa upande wa shule ya msingi wanajenga madarasa manne pamoja na matundu ya vyoo ambapo gharama ya ujenzi itakuwa sh milioni 131 huku ujenzi wa shule ya sekondari wanatarajia kutumia kiasi cha sh.224.5 Kwa àjili ya ujenzi wa madarasa 12, maabara na matundu ya vyoo.


"Mradi huu ulikuwa unajumuisha ujenzi wa bweni kwa ajili ya wanafunzi wanaoishi maeneo ya mbali lakini mpaka sasa hatujaweza kuletewa fedha sh milioni 44.5" alisema ofisa elimu huyo.


Kwa upande wake fundi mkuu wa ujenzi wa shule ya msingi Paul Allen alisema kuwa ndani ya siku nane anataraji kukamilisha hatua ya kupauwa na hivyo kumaliza ndani ya wakati ujenzi wake.


"Kwa hatua niliyofikia majengo haya ya shule yatakamilika ndani ya siku nane na kabla ya muda huo wa wiki tatu ulizosema mkuu wa mkoa nitakuwa nimeshakabidhi majengo haya kwa ajili ya kutumika" alisema Allen

Post a Comment

0 Comments