Ticker

6/recent/ticker-posts

MSIGWA- TUMIENI FURSA ZA BANDARI NA MAZIWA MAKUU, SERIKALI INAAHIDI KUWAUNGA MKONO.


Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, Gerson Msigwa akizungumza wakati timu ya maofisa wa habari kutembelea katika bandari ya Tanga baada ya kumaliza kikao kazi chao kwa siku ya pili mkoani Tanga na kwenda kujionea maendeleo ya ujenzi wa mradi mkubwa unaoendelea.


*****************

Na Hamida Kamchalla, Tanga.
SERIKALI nchini imelenga kuimarisha miundombinu ya bahari na maziwa ili kuinua biashara kupitia bandari tatu pamoja maziwa matatu ambayo yatakwenda kufungua fursa kwa Watanzania.


Kauli hiyo imetolewa na Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, Gerson Msigwa wakati timu ya maofisa wa habari kutembelea katika bandari ya Tanga baada ya kumaliza kikao kazi chao kwa siku ya pili mkoani Tanga na kwenda kujionea maendeleo ya ujenzi wa mradi mkubwa unaoendelea.


Msigwa alisema serikali inafungua fursa za kibiashara huku ikiwataka wafanyabiashara na wananchi mbalimbali wanaotumia bandari na maziwa kutumia fursa hizo na kuahidi kuwaunga mkono.


"Kama serikali tunafungua fursa za kibiashara, na nipende kutoa wito kwamba serikali iko tayari kuwaunga mkono wafanyabiashara na watu balimbali kutumia fursa hizi kukuza biashara, bandari hii ni lango la biashara la nchi, na sisi tuna bahati ya kuwa katika bahari ambayo tuna bandari hii inayotegemewa na nchi takribani nane" alisema.


"Kwahiyo wafanyabiashara wa nchi hii tusilale usingizi tukawaachia wengine wakaja kutumia hii fursa kwa kiasi kikubwa, lakini pia kubwa zaidi kuna miradi inakuja nchini kwetu, tuchangamkie hizi fursa twende tukapate ajira, tufanye biashara na viwanda vinavyokuja kuwekwa kwenye nchi yetu" alisema.


Aidha Msigwa aliwataka wananchi kuunga mkonojuhudi za serikali kwa kuitumia vema miundombinu ambayo inawekwa na serikali kwa nia ya kuwasaidia wananchi badala ya kuharibu kwa maslahi yao binafsi na kuumiza wengine.


"Lakini pia wananchi tuunge mkono juhudi za serikali kwa kuhakikisha kwamba miundombinu hii inayojengwa, inalindwa, kwasababu tumekuwa na tabia sisi Watanzania baadhi yetu tunakwenda kuharibu miundombinu" alibainisha.


"Ni muhimu sana kwetu sisi tukaona kwamba kinachofanyika kinatokana na kodi zetu, ni fedha zetu zinazotoka mifukoni mwetu nna mali hizi ni zetu sisi wenyewe, kwahiyo ni lazima tuwe kipaumbele kuhakikisha tunaulinda na akitokea mtu anayehujumu tia taarifa, viongozi na vyombo vya usalama wapo, toa taarifa na hatua zitachukuliea" alisisitiza Msigwa.


Alifafanua kwamba kuwapeleka maofisa habari kwenye miradi mikubwa inalenga kuwapa uelewa zaidi juu ya miradi hiyo ambayo inatekelezwa katika kipindi cha awamu ya sita ili wananchi wapate kuelewa kibachofanywa na serikali.


"Maofisa habari hawa ndiyo wanafanya Mawasiliano kati ya serikali na wananchi, keahiyo, kando na kikao kazi chetu cha utendaji tunachofanya hapa Tanga, tumeona tuwalete katika moja ya miradi yetu ambayo inatekelezwa na serikali ya awamu ya sita katika bandari hii" alisema Msigwa.


Hata hivyo alibainisha kwamba itambulike dhahiri na wananchi kwamba katika kuinua uchumi wa bluu, kuna kazi zinafanyika kwa Mkoa wa Tanga, lakini pia kwenye maziwa ambayo yamefikiwa katika Mikoa ya Kigoma ziwa la Kalema, ziwa Tanganyika na Victoria mkoani Mwanza ambako maofisa wa habari walitembelea.


Naye Mhandi wa mradi wa bandari ya Tanga Hamisi Kipalo alisema bandari ya Tanga Ina mradi mkubwa wenye awamu mbili ambazo zinaendelea kutekelezwa wakati awamu ya kwanza imekwisha na ya pili ambao ni kuboresha ujenzi wa gati namba 1 na 2 lenye uefu wa mita 450 na upana wa mita 150 iko asilimia 43.


"Kwenye mkataba kuna kipengele kinasema, Mkandarasi anatakiwa kukabidhi kipande cha mira 150 kwanza, natumaini kwenye mwezi wa sita tutakabidhiwa kipande hiki" alisema Kipalo.

Post a Comment

0 Comments