Ticker

6/recent/ticker-posts

NIMR: MAKAMU WA RAIS DKT.PHILIP MPANGO KUFUNGUA KONGAMANO LA 31 MEI 17,2022



**********************

Na Magrethy Katengu

Taasisi ya utafiti wa magonjwa ya binadamu (NIMR) inatarajia kufanya kongamano la 31 la kisayansi mwaka huu kuanzia mei 17-19 Jijini Dar es salaam ambapo makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Philip Mpango anatajiwa kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi.

Akizungumza na waandishi wa habari mkurugenzi Mkuu wa NIMRI Profesa Yunus Mgaya amesema kwamba kongamano hilo linalenga kusambaza matokeo ya tafiti za afya zinazofanywa na watafiti wa NIMR na wadau wengine waliopo ndani na nje ya Nchi ,nakwamba zimebeba ujumbe usemao"Ushiriki wa Sekta Mbalimbali katika Afya:ajenda ya kuimarisha Mifumo ya afya kufikia huduma ya afya Kwa Wote".

"Nafurahi kueleza kuwa mafanikio makubwa yanatokana na kuratibu makongamano kama haya,yanaleta chachu ya mwendelezo na mwaka huu (2022) tunaratibu kongamano la 31,litafanyika kwa siku ambapo atazindua rasmi tarehe 17 /05/2022 na Makamu wa rais Daktari.Philip Mpango katika kituo cha kimataifa cha Julius Nyerere Dar see salaam" amesema Profesa Mgaya.

Ameendelea kufafanua kwamba kupitia kongamano hilo inasaidia kuibua na kubainisha maeneo muhimu ya afya yanayohitaji hatua za haraka za kitafiti zitakazoleta mabadiliko ya sera ,miongozo,mifumo ya tiba na utendaji Kwa lengo la kuboresha afya ya jamii.

"Tuanapozungumzia huduma ya afya kwa wote tunamaanisha wananchi wote waweze kufikiwa na huduma muhimu za afya zinazohusisha uelimishaji kuhusu afya bora,Kinga,matibabu,utunzaji wa dawa na hatimaye uboreshwaji wa maisha ya mtanzania Kwa ujumla,kongamano hili linashirikisha watalaam zaidi ya miatatu kutoka katika taasisi mbalimbali za kitaifa nchini naza kimataifa wakiwemo watafiti na watunga sera" amesisitiza Mkurugenzi huyo wa NIMRI.

Hata hivyo ameongeza kwamba maandiko 260 yakisayansi yanatarajiwa kuwasilishwa katika kongamano hilo kupitia mada ndogondogo zitakazohisu Magonjwa mbalimbali ,vichocheo vyake na ufanisi katika mfumo wa afya kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo Magonjwa ambukizi,tiba asili,usugu wa dawa katika tiba ya magonjwa na mifumo ya udhibiti wa magonjwa.

Maeneo mengine ni afya ya mazingira na Mabadiliko ya Tabianchi, Magonjwa yasiyoambukiza,huku eneo jingine ni changamoto za afya zitokanazo na janga la UVIKO 19 ,Lishe,Afya ya mama,mtoto na vijana,magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele,pamoja na udhibiti na usimamizi wa tafiti za Tiba.

Hata hivyo amesema Jumla ya maandiko 260 ya kisayansi yanatarajiwa kuwasilishwa katika kongamano hilo kupitia mada zitakazohusu magonjwa mbalimbali na vichocheo vyake na ufanisi katika mfumo wa afya ikiwemo magonjwa ambukizi yanayoibuka na yabayojitokeza baada ya kutokomezwa,tiba asili,magonjwa yasiyoambukiza

Kwa upande wake mkurugenzi mratibu wa taarifa na mawasiliano ya kitafiti Dr Ndekya Oriyo amesema kwamba Nchi mbalimbali zimethibitisha kushiriki kwenye kongamano hilo ikiwemo Marekani,Ujerumani,Uganda,Uingereza,Senegari,Afrika Kusini,ambapo litasaidia kujadili kwa pamoja changamoto mbalimbali zinazoikumba sekta ya afya.

Aidhha kongamano hilo litaambatana na maonyesho yatakayolenga kutoa ufahamu zaidi juu ya kazi zinazofanywa na taasisi za afya,watoa huduma na wadau wengine wa nje ya sekta ya afya baadhi ya wadau hao niTMDA,MUHAS,NMB hivyo watu wote wanakaribishwa kufuatilia kupitia vyombo vya habari

Post a Comment

0 Comments