Ticker

6/recent/ticker-posts

OFISI YA WAZIRI MKUU, PSSSF YAKUTANA NA JUKWAA LA WAHARIRI TANZANIA (TEF) KUJADILI KANUNI MPYA YA MAFAO YA PENSHENI

Mkurugenzi wa Idara ya Hifadhi ya Jamii Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Festo Fute akizungumza na Wahariri wa wakati wa mkutano wenye lengo la kujua kanuni mpya ya mafao ya mfuko wa pensheni uliofanyika jijini Dodoma jana.
Kamishna, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Nyanda Shuli akitoa mada kuhusu kanuni mpya ya mafao ya mfuko wa pensheni.
Mkurugenzi wa Adhari kutoka PSSSF, Ansiger Mushi akichangia jambo kwenye mkutano huo.


Mwanasheria wa NSSF, Frank Mgeta akichangia jambo kwenye mkutano huo.




Meneja Matekelezo kutoka PSSSF, Victor Kikoti akizungumza kwenye mkutano huo.
Meneja Uhusiano Elimu kwa Umma kutoka NSSF, Lulu Mengele akichangia jambo kwenye mkutano huo..
Wahariri wa vyombo vya habari wakiwa kwenye mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.


Mkutano ukiendelea











Na Dotto Mwaibale, Dodoma



OFISI ya Waziri Mkuu kupitia Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma, (PSSSF) wamekutana na Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) kwa ajili ya kujadili kanuni mpya ya mafao ya pensheni nchini kwa lengo ya kuisaidia Serikali kupeleka ujumbe huo kwa jamii.

Akitoa mada katika mkutano huo wa siku moja uliofanyika jijini Dodoma Kamishna, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Nyanda Shuli alisema mkutano huo na wadau wa vyombo vya habari ni wa muhimu kwa ajili ya kufikisha ujumbe kwa wananchi ili wazijue kanunu hizo mpya.

Alisema kazi ya kubadilisha kanuni hizo ilifanyika kwa ushirikiano wa Wadau wa tatu (Serikali, TUCTA na ATE) na kuwezesha kupatikana kwa kanuni bora na endelevu.

Shuli alisema Mtaalam Elekezi alipendekeza baadhi ya kanuni zitumike kwa mifuko yote miwili wa NSSF na PSSSF yaani Malipo ya Mkupuo asilimia 25 kwa Mifuko yote,Kikokotoo limbikizi cha 1/580 na Makadirio ya miaka 12.5 ya kuishi baada ya kustaafu.

Alisema kanuni hiyo inatoa kiwango cha mkupuo cha asilimia 33, na kutumia wastani wa mishahara bora ya miaka mitatu ndani ya miaka kumi kabla ya kustaafu.

Aidha Shuli alisema faida ya kanuni hiyo mpya inaongeza kiwango cha mkupuo kutoka asilimia 25 iliyolalamikiwa mwaka 2018 hadi asilimia 33, wanachama wote wa mifuko watanufaika na ongezeko hilo ambapo malipo ya mkupuo yatapanda kwa 81% ya wanachama na malipo ya pensheni yataongezeka kwa 19% ya wanachama na inaongeza pensheni ya mwezi kutoka asilimia 50 ya sasa hadi asilimia 67 kwa wanachama wa PSPF na LAPF.

Mwanasheria wa NSSF Frank Mgeta akizungumza katika mkutano huo alisema Sheria ya Mfuko wa na Hifadhi ya Jamii ya mwaka 2018 inamtaka mwajiri kuwasilisha michango ya wafanyakazi na ni kosa la kisheria kwa mwajiri kushindwa kuwasilisha michango hiyo na anapobainika sheria itachukuliwa dhidi yake ikiwa ni kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.


Post a Comment

0 Comments