Ticker

6/recent/ticker-posts

PSPTB YATAKA WANAOFANYA KAZI ZA UNUNUZI NA UGAVI WASIO NA SIFA STAHIKI WAFUKUZWE



****************

Na Magrethy Katengu

Bodi ya Wataalamu wa manunuzi na ugavi (PSPTB) imewataka waajiri wote sekta ya umma na binafsi kuwaondoa watumishi kwenye kitengo cha ununuzi na ugavi maafisa wote wasio na sifa za kitaalam kwa mujibu wa muongozo wa usajili wa PSPTB na muundo wa Utumishi wa kada zilizopo chini ya wizara ya fedha na mipango waraka namba 3 wa mwaka 2015.

Agizo hilo amelitoa leo mkurugenzi Mtendaji wa Bodi hiyo Bw. Godfred Mbanyi wakati akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam ambapo amesema ukaguzi uliofanyika imebainika bado kuna waajiri wanaajiri watu kufanya kazi za ununuzi na ugavi bila usajili wa PSPTB hali ambayo ni kinyume Cha sheria.

"Katika kutekeleza jukumu hilo kisheria, PSPTB imebaini bado kuna Waajiri wanaajiri watu kufanya kazi za ununuzi na jgavi bila usajili wa bodi yetu,kupitia taarifa ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali (CAG) na Mamlaka ya ununuzi wa Umma (PPRA) zimeonyesha ukiukwaji wa sheria katika kitengo cha kuwa na Wakuu wa vitengo wasio na sifa za kitaaluma" amesema Bw.Mbanyi.

Sanjari na hayo ameongeza Kwa kusema Pia taarifa hizi zimebaini mapungufu makubwa kwenye ukidhi wa Sheria ya ununuzi wa umma na kanuni zake nakupelekea hasara kwa Serikali ,hivyo PSPTB inawataka wataalamu wote wanaofanya kazi kwenye kitengo cha ununuzi na ugavi kuhakikisha wanafanya kazi kwa kuzingatia maadili ya taaluma yao Kwa mujibu wa muongozo wa maadili ya kazi ya ununuzi na ugavi wa Bodi hiyo.

Hata hivyo ameendelea kuwaagiza wataalam wa Ununuzi na ugavi wa sekta binafsi na umma kufanya kazi kwa weledi na kutoa ushauri Kwa umakini bila hofu ili kupata thamani ya fedha.

" Kuanzia Mei 17 tunaanza kutoa elimu Kwa umma kupitia vyombo vya habari,tunaomba pia Waandishi wa habari mtusaidie kufikisha elimu hii ili tuweze kudhibiti upotevu wa fedha nyingi ambazo zimekua zikipotea kutokana na kukosekana Kwa weledi wa kazi Kwa baadhi ya wafanyakazi wa manunuzi na ugavi" amesisitiza mkurugenzi mtendaji huyo wa PSPTB'alisema Mbanyi

Aidha,Mbanyi amesema kifungu cha 46 kimezuia kuajiri au kufanya kazi za ununuzi na ugavi kwa mtu yeyote ambaye hajasajiriwa na bodi ya PSPTB na adhabu yake kwa atakayekiuka kifungo hicho ni kosa la jinai na adhabu yake ni kifungu kisichozidi miaka miwili au faini isiyozidi milioni mbili au vyote kwa pamoja.

Hata hivyo,Mbanyi amewataka wataalam wote waofanya kazi kitengo cha Ununuzi na Ugavi kuhakikisha wanafanya kazi kwa kuzingatia maadili ya taaluma yao kwa mujibu wa maadilh' ya PSPTB namba 365/2009.

Post a Comment

0 Comments