Ticker

6/recent/ticker-posts

SERIKALI KUSHIRIKIANA NA WABUNIFU KUTANGAZA UTALII KIDIGITALI

Mkurugenzi kitengo cha mawasiliano wizara ya Mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika mashariki Balozi Mindi Kasiga akizungumza

Donald Nsanyiwa Mtaalam wa kodi kutoka KPMG akizungumza na waandishi wa habari katika wiki ya ubunifu inayoendelea Jijini Dar es Salaam
Washiriki katika wiki ya ubunifu


**************************

Na Magrethy Katengu

Serikali imesema itahakikisha inashirikiana na wabunifu wa kitanzania kwa kutumia njia za kidigitali kutangaza utalii ili kuendana na Dunia inayoenda kasi kisayansi na kiteknolojia na kusaidia kuvutia watalii kwa wingi na pato la Taifa kuongezeka

Ameyasema hayo leo Jijini Dar es salaam Mkurugenzi kitengo cha mawasiliano wizara ya Mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika mashariki Balozi Mindi Kasiga katika wiki ya ubunifu Tanzania inayoratibiwa na Wizara ya sayansi na teknolojia kwa kushirikiana na COSTECH, ubalozi wa uholanzi na UNDP kupitia program yake ya Ubunifu Funguo ambapo amesema kuna umuhimu wa kutumia wabunifu kutengeneza mazingira mazuri ya kutangaza utalii ndani na nje ya nchi

"Sasa ni wakati wa kubadilika kuendana na mazingira ya Sasa siyo kuendelea kutangaza utalii Kwa kutumia njia zilezile za kizamani hivyo tunapaswa tumuige Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassani alichokifanya Kwa kutumia filamu ya royal tour kuonyesha vivutio vya Utalii vilivyopo Nchini Jambo ambalo litaleta matokeo chanya siku za mbele"alisema Balozi Mindi

Naye Donald Nsanyiwa Mkurugenzi wa kodi Amesema wa wabunifu wanakumbana na changamoto mbalimbali katika masuala ya kikodi ikiwemo kukosa mashine ya EFD risiti wakati kufanya shughuli zao.

Kwa upande wake mwanzilishi mbunifu wa kampuni ya safari waleti Ididy John ambapo amesema kampuni hiyo imebuni mfumo unaoendeshwa Tanzania na nje ya mipaka unaomwezesha mtalii kupanga safari yake mapema kabla ya kusafiri ambapo anaweza kutumia mfumo huo kulipa kidogo kidogo kabla ya safari

Hata hivyo ameiomba serikali kuziangalia kampuni changa zinazoanza Kwa kuzipunguzia Kodi Kwa kipindi kifupi kutokana na changamoto inayowakabili wanapokuwa wanaanza wakati mwingine kuwa na uhaba wa fedha

Post a Comment

0 Comments