Ticker

6/recent/ticker-posts

TALGWU YAMPONGEZA RAIS SAMIA SULUHU KWA KUTOA AHADI YA NYONGEZA YA MISHAHARA



*********************************

Na Magrethy Katengu

Chama Cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania(TALGWU) kimempongeza rais Samia Suluhu Hassani kwa kuahidi kuongeza nyongeza ya mishahara kwa Wafanyakazi ambapo ahadi hiyo itaanza kufanyiwa kazi julai mwaka huu hivyo aliwaomba wawe wastahimilivu.

Akizungumza wakati wa kutoa tamko hilo Katibu Mkuu wa TALGWU  Bw.Rashidi Mtima amesema kwamba ahadi alizozitoa rais Samia Suluhu Hassan katika maadhimisho hayo ikiwemo kuahidi kuongeza mishahara ya Wafanyakazi zimejenga ari ya kufanya kazi na kuleta matumaini mapya kwa Wafanyakazi ambayo yalikua yamepotea kwa miaka mingi.

"Tunamshukuru kwa kutuhakikishia nyongeza ya mishahara ambapo ni muda mrefu sasa Watumishi wa Umma hawajapandishiwa mishahara,hiki kilikua kilio chetu Cha muda mrefu ambapo Sasa kwa sasa hali ya gharama za kupanda vitu bei inazidi kuongezeka na mshahara wanaopokea haukidhi mahitaji yao "Alisema Mtima

Nakuongeza kuwa" tunatoa shukrani zetu za dhati kwa Mheshimiwa Rais Samia kwa kuundwa kwa bodi yakupitia kima Cha chini Cha Mishahara iliyopo sasa na kuagiza Wizara zinazohusika kuiwezesha bodi hiyo ili kutekeleza majukumu take ipasavyo.

Pia ameendelea kubainisha kwamba wamefurahishwa na kitendo Cha rais Samia kusikiliza kilio Cha muda mrefu kuhusu Watumishi walioondolewa kazini kwa vyeti vya kughushi (Feki) hivyo TALGWU Kama chama kwa kupitia Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Nchini TUCTA wamekua wakiomba kwa muda mrefu serikali kuliangalia kundi hilo la Watanzania ambao walitumika kwa uadilifu,ambapo ameagiza Wizara ya Fedha na Mipango kushughulikia na kuwalipa stahiki zao zinazotokana na makato ya mishahara.

Katibu Mkuu huyo wa TALGWU kupitia tamko hilo amesema kwamba wanaishukiru serikali kwa kuagiza mifuko ya hifadhi ya jamii na maafisa Utumishi kuhakikisha wanashughulikia haki na stahiki za Watumishi wanaotarajiwa kustaafu ndani ya miezi sita ili pindi inapofika Mtumishi anastaafu mafao take yawe tayari hali ambayo inaondoa usumbufu kwa wanachama kwani wengi wao hutegemea mafao kwa ajili ya kuendeleza maisha yao.

Amemaliza kwa kusema kuwa TALGWU imefurahishwa na kitendo Cha serikali kuingilia Kati nakutoa maelekezo yakukemea kwa Wafanyabiashara wanaopandisha bei za bidhaa holela hali ambayo inapunguza uwezo wa Wafanyakazi kiweza kununua bidhaa na kukidhi mahitaji take.

Post a Comment

0 Comments