Ticker

6/recent/ticker-posts

WAZIRI GWAJIMA AZINDUA BODI YA MAGAVANA YA TAASISI YA USTAWI WA JAMII

Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima akizungumza katika uzinduzi wa Bodi uliofanyika leo Mei 24,2022 katika Taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam.Mwenyekiti wa Bodi ya Magavana wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii , Mhe.Sophia Simba akizungumza katika uzinduzi wa Bodi hiyo uliofanyika leo Mei 24,2022 katika Taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam. Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Zainab Chaula akizungumza katika uzinduzi wa Bodi hiyo uliofanyika leo Mei 24,2022 katika Taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam. Mkuu wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii Dkt.Joyce Nyoni akizungumza katika uzinduzi wa Bodi hiyo uliofanyika leo Mei 24,2022 katika Taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam. Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe.Amon Mpanju akizungumza katika uzinduzi wa Bodi hiyo uliofanyika leo Mei 24,2022 katika Taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam. Baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya Magavana wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii wakiwa katika uzinduzi wa Bodi hiyo uliofanyika leo Mei 24,2022 katika Taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam. Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima akikabidhi vifaa vya kazi kwa Wajumbe wa Bodi ya Magavana wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii katika uzinduzi wa Bodi hiyo uliofanyika leo Mei 24,2022 katika Taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam.


Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima akikata keki kuashiria uzinduzi wa Bodi ya Magavana wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii uliofanyika leo Mei 24,2022 katika Taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

***********************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima ameitaka Bodi ya Magavana ya Taasisi ya Ustawi wa Jamii kuhakikisha Chuo cha Ustawi wa Jamii kinatoa wahitimu wa Ustawi wa Jamii ambao watakwenda kusaidia kupunguza changamoto ya watu wenye matatizo ya kisaikolojia.

Dkt. Gwajima ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa Bodi ya Magavana wa taasisi ya Ustawi wa jamii ambapo amesema kazi ya wanataaluma wa ustawi ni kuhakikisha wanatoa elimu kwenye jamii ili kuweza kuibadilisha saikoloji kwa watu kutaka kujinyonga,ndoa kuvunjika.

"Kaangalieni changamoto mnazoweza kuzifanyia kazi kwa haraka mzifanyie kazi ili Bodi yenu iweze kuonyesha matokeo ya haraka Bodi yenu iweze kuonyesha matokeo makubwa". Amesema Waziri Gwajima.

Aidha, Dkt Gwajima amesema kwa sasa Serikali ipo katika mkakati wa kuja na usajili kwa wanataaluma ya ustawi wa jamii ambapo wataweza kufungua Kliniki zitakazoweza kuweza kuwasaidia watu wanaokumbana na changamoto za matatizo ya saikolojia .

Sanjari na hayo Dkt Gwajima pia ameitaka bodi hiyo kufanya kazi kwa kasi zaidi ili kuweza kumsaidia Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania,Samia Suluhu Hassani Katika adhima yake ya kuwaletea maendeleo Watanzania.

Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Mhe.Sophia Simba amesema atahakikisha kunaanzishwa kwa madawati ya ustawi kila kata ili kuweza kusaidia jamii inayohitaji wataalamu wa Ustawi.

Nae Mkuu wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii Dkt.Joyce Nyoni amesema mabweni yaliyopo yanaweza kuhudumia watu zaidi ya 270 kati ya wanafunzi zaidi ya 4400 waliopo kwa sasa.

Post a Comment

0 Comments