Ticker

6/recent/ticker-posts

WIZARA YA MAMBO YA NJE KUENDELEA KUTOA ELIMU KUHUSU FURSA ZITOKANAZO NA ENEO HURU LA BIASHARA AFRIKA

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imejipanga kuendelea kutoa elimu kwa umma na wadau mbalimbali hapa nchini kuhusu fursa zitokananzo na Eneo Huru la Biashara Barani Afrika (African Continental Free Trade Area-AfCFTA) ili kuwawezesha kuzichangamkia kwa manufaa yao na nchi kwa ujumla.

Kauli hiyo imetolewa leo tarehe 29 Mei 2022 jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk wakati akifungua rasmi Warsha ya Kueleimisha na Kujenga Uwezo kwa Wajumbe wa Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama kuhusu Mkataba ulioanzisha Eneo Huru la Biashara la Afrika.

Mhe. Balozi Mbarouk amesema kuwa, watanzania wana kila sababu ya kuchangamkia fursa zinazotokana na Mkataba wa AfCFTA na kunufaika nazo kwa kuwa Tanzania ni mwanachama kamili wa mkataba huo baada ya Bunge kuuridhia mnamo mwezi Januari 2022. Fursa hizo ambazo ni pamoja na Biashara, Ajira, Uwekezaji, Teknolojia zitainufaisha nchi kwa kukuza pato la Taifa kutokana na eneo kubwa la soko, kukuza viwanda, ongezeko la biashara ndani ya Afrika na kuongezeka uzalishaji na mnyororo wa thamani.

“Ili kuwawezesha wadau kutambua na kutumia fursa za AfCFTA, Serikali imejipanga kuwa na mkakati endelevu wa kutoa elimu kwa umma. Tayari Serikali imeanza kutoa elimu na kujenga uwezo kwa wadau kwa makundi. Tayari Warsha za aina hii zimefanyika Zanzibar, Dar es Salaam, Morogoro na Mwanza na zimehusisha Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi, Watumishi wa Umma na Sekta Binafsi” amesema Mhe. Mbarouk.

Ameongeza kusema kuwa, AfCFTA ni muhimu kwa Tanzania katika kupanua wigo wa soko la bidhaa na huduma nje ya soko la EAC na SADC na kwamba Wizara inatumia fursa ya AfCFTA kutekeleza mikakati ya Diplomasia ya Uchumi ya kuvutia wawekezaji nchini ilikuzalisha na kuuza kwenye soko la AfCFTA.

Pia alitumia fursa hiyo kuwaomba Wajumbe wa Kamati hiyo kuwa Mabalozi kwenye suala hilo na kushirikiana na Serikali kuendelea kutoa elimu kwa wadau ili Tanzania itumie ipasavyo fursa zitokanazo na ushiriki wake katika AfCFTA.

“Nina imani kuwa kupitia warsha hii, kila mmoja wetu atakuwa amepata elimu ya kutosha kuhusu mkataba wa AfCTA pamoja na fursa zake na mtakuwa mabalozi wazuri kwenye suala hili katika kushirikiana na Serikali” alisisitiza Balozi Mbarouk.

Akiwasilisha mada kuhusu Mkataba wa AfCFTA, Mkurugenzi wa Idara ya Biashara, Uwekezaji na Sekta za Uzalishaji katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Bernard Haule amesema nchi 54 za Afrika zimesaini Mkataba huo na tayari nchi 43 ikiwemo Tanzania zimeuridhia. Amesema malengo ya kuanzishwa mkataba huo ni pamoja na kutengeneza soko moja la uhakika la kuhimili vishindo vya dunia; kujenga na kukuza uzalishaji na uwezo wa uchumi wa viwanda barani Afrika na kuweka msingi utakaowezesha kuwa na umoja wa forodha wa Afrika.

Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Mhe.Vincent Mbogo ameipongeza na kuishukuru Wizara kwa kundelea kutoa elimu na kushauri jitihada zaidi zitumike ili kuwafikia wananchi wa mijini na vijijini. Pia amesisitiza umuhimu wa Serikali kuwa na takwimu sahihi za mahitaji ya soko na zile za uzalishaji ili kuwe na uwiano na mwendelezo kwenye ufanyaji biashara. Vilevile elimu ya uzalishaji wa bidhaa bora na zenye viwango itolewe ili kukidhi matakwa ya Soko hilo.

“Naipongeza Wizara kwa hatua hii. Hata hivyo bado mna kazi kubwa ya kuwafikia watu wa mijini na vijijini ili kuwaeleimisha kuhusu fursa zitokanazo na soko hili muhimu. Tumieni njia mbalimbali kutoa elimu hii ikiwemo vyombo vya habari kama radio, televisheni na mitandao ya kijamii ili elimu hii iwafikie wananchi kwa wingi” alisema Mhe. Mbogo.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (Mb) akifungua rasmi warsha ya siku moja iliyoendeshwa na Wizara kwa Wajumbe wa Kamati ya ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama kuhusu Mkataba wa Eneo Huru la Biashara la Afrika (AfCFTA). Warsha hiyo imefanyika jijini Dodoma tarehe 29 Mei 2022. Kulia ni Kaimu Katibu Mkuu wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Fatma Mohammed Rajab

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Mhe. Vincent Mbogo (Mb) (kushoto) akiwa na Katibu wa Kamati wakati wa Warsha iliyotolewa na Wizzara kuhusu Eneo Huru la Biashara la Afrika

Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Fatma Mohammed Rajab nae akizungumza wakati wa Warsha iliyotolewa na Wizara kwa Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama



Mkurugenzi wa Idara ya Biashara, Uwekezaji na Sekta za Uzalishaji katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Bernard Haule akiwasilisha mada ya kujenga uwezo kwa Wabunge kuhusu Eneo Huru la Biashara la Afrika kwa Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (hawapo pichani)
Sehemu ya Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama wakifuatilia uwasilishwaji wa mada kuhusu Eneo Huru la Biashara la Afrika

Sehemu nyingine ya Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama

Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama wakati wa warshailiyotolewa kwao kwa lengo la kuwaelimisha na kuwajengea uwezo kuhusu Soko Huru la Biashara la Afrika. Kushoto ni Mhe. Mustafa Mwinyikondo Rajab (Mb) na kulia ni Mhe. Felista Njau (Mb)

Wakurugenzi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakishiriki warsha. Kutoka kushoto ni Balozi Stephen Mbundi, Mkurugenzi wa Idara ya Siasa, Ulinzi na Usalama, Bw. Lawrence Mwesiga, Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Biashara, Uwekzaji na Sekta za Uzalishaji na Balozi Agnes Kayola, Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda

Sehemu nyingine ya Wakurugenzi na wawakilishi kutoka Wizarani. Kutoka kushoto ni Bw. Marobe Wama, Msaidizi wa Kaimu Katibu Mkuu, Bw. Magabilo Murobi, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Diplomasia ya Uchumi na Bi. Linda Rujweka, Afisa TEHAMA

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Justine Kisoka akifuatilia warsha

Mkurugenzi wa Idara ya Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Jamii katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Eliabi Chodota akifafanua jambo wakati wa warsha kuhusu Soko Huru la Biashara la Afrika

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Mhe. Vincent Mbogo (Mb) akishauri jambo kwa Wizara wakati wa warsha kuhusu Soko Huru la Biashara la Afrika

Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Mhe. Muharami Mkenge (Mb) akichangia jambo wakati wa warsha

Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Mhe. Abeid Ramadhani (Mb) nae akichangia jambo

Mjumbe wa Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Mhe. Joseph Mkindi (Mb) akitoa ushauri kwa Wizara kuhusu namna ya kunufaika na Eneo Huru la Biashara la Afrika

Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Mhe. Zahor Mohamed Haji (Mb) akichangia jambo kuhusu Eneo Huru la Biashara la Afrika

Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Mhe. Cosato Chumi (Mb) akichangia hoja

Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Mhe. Janeth Masaburi (Mb) akitoa mchango wake wakati wa warsha hiyo

Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Mhe. Abdi Hija Mkasha (Mb) nae akichangia jambo

Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Mhe. Fakharia Shomar Khamis (Mb) akitoa hoja kuchangia mada kuhusu Eneo Huru la Biashara la Afrika


Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Mhe. Mustafa Mwinyikondo Rajab (Mb) wakati wa warsha kuhusu Eneo Huru la Biashara Barani Afrika

Afisa Mratibu wa shughuli za Bunge katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Joshua Mponera akifuatilia matukio wakati wa warsha kwa Wabunge kuhusu Eneo Huru la Biashara la Afrika




Post a Comment

0 Comments