Ticker

6/recent/ticker-posts

ADC YATOA NENO MCHAKATO WA KATIBA MPYA

KATIBU Mkuu wa Chama cha Aliance Demokratc Change (ADC) Doyo Hassan Doyo akizungumza na wananchi wa Kata ya Mabanda Jimbo la Handeni mjini.
KATIBU Mkuu wa Chama cha Aliance Demokratc Change (ADC) Doyo Hassan Doyo kulia akigaiawa kadi kwa wanachama wapya waliojiunga na chama hicho mara baada ya kuzindua tawi hilo
KATIBU Mkuu wa Chama cha Aliance Demokratc Change (ADC) Doyo Hassan Doyo kulia akigaiawa kadi kwa wanachama wapya waliojiunga na chama hicho mara baada ya kuzindua tawi hilo
KATIBU Mkuu wa Chama cha Aliance Demokratc Change (ADC) Doyo Hassan Doyo kulia akigaiawa kadi kwa wanachama wapya waliojiunga na chama hicho mara baada ya kuzindua tawi hilo


*************************

KATIBU Mkuu wa Chama cha Aliance Demokratc Change (ADC) Doyo Hassan Doyo amesema suala la CCM kuzungumzia mchakato wa Katiba mpya kwamba imeridhia na wanasubiri Serikali ione namna gani linafufuliwa wamelipokea kwa mikono miwili.

Doyo aliyasema hayo leo mjini Handeni wakati akifungua Tawi Mtaa wa Mabanda Kata ya Mabanda Jimbo la Handeni Mjini na kufanikiwa kupata wanachama zaidi ya 60 ambao walichukua kadi ya ADC huku akiwashukuru wananchi kwa kukiunga mkono chama hicho .

Alisema hivi sasa wanasubiri Serikali iweze kuona namna gani jambo hilo linafufuliwa ili mchakato uanze huku akieleze wamelipokea kwa furaha japokuwa hawaamini kwamba CCM wana nia thabiti ya kujenga mifumo ya katiba ambayo watanzania wanaihitaji.

Alisema kutokana na wasiwasi huo wanaitaka Serikali ya CCM iweze kutoa tamko la haraka la kukubali huo mfumo na kwamba unaanza lini na mchakato wake utakuwaje kutokana na kwamba ni suala rahisi sana .

“Kwani sheria ya mabadiliko ya katiba imeshatungwa hivyo ni kuifufua tu na bunge bado linakaa na tunaamini kama Serikali ipo makini na suala ka katiba mpya na CCM imebariki hivyo itoa tamko haraka ni lini mchakato wa katiba mpya utaanza”Alisema Katibu Mkuu huyo.

Hata hivyo alisema suala la katiba mpya kwa watanzania ni muhimu sana na ndio maana wamekuwa wakilipigia kelele mara kwa mara ili kuhakikisha inapatikana.

Katika hatua nyengina Katibu huyo Mkuu aliwataka wananchi wa Kata hiyo kuhakikisha wanajitokea ,kwa wingi kuhesabiwa wakati wa zoezi la Sensa ya watu na Makazi linatalofanyika mwezi Agosti mwaka huu hapa nchini kutokana na kwamba ni tukio muhimu kwa nchi.


Post a Comment

0 Comments