Ticker

6/recent/ticker-posts

KATIBU MKUU UVCCM AONGOZA MATEMBEZI KUHAMASISHA SENSA YA WATU NA MAKAZI

Katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa, Bw.Kenani Kihongosi akiongoza vijana kwenye matembezi kutoka katika Uwanja wa Benjamini Mkapa mpaka kwenye viwanja vya Muembe Yanga Temeke Jijini Dar es salaam katika uzinduzi wa Uhamasishaji wa SENSA ya Watu na Makazi ambayo itakuwa endelevu kwa nchi nzima.SENSA ya Watu na Makazi inatarajia kufanyika Agosti 23,2022. Baadhi ya jumbe za uhamasishaji wa SENSA zilizobebwa na vijana kwenye kwenye matembezi kutoka katika Uwanja wa Benjamini Mkapa mpaka kwenye viwanja vya Muembe Yanga Temeke Jijini Dar es salaam katika uzinduzi wa Uhamasishaji wa SENSA ya Watu na Makazi ambayo ambayo itakuwa endelevu kwa nchi nzima.SENSA ya Watu na Makazi inatarajia kufanyika Agosti 23,2022. Baadhi ya Vijana wakitanzania wakiwa kwenye matembezi ambayo yameanzia katika Uwanja wa Benjamini Mkapa mpaka kwenye viwanja vya Muembe Yanga Temeke Jijini Dar es salaam katika uzinduzi wa Uhamasishaji wa SENSA ya Watu na Makazi ambayo itakuwa endelevu kwa nchi nzima.SENSA ya Watu na Makazi inatarajia kufanyika Agosti 23,2022. Katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa, Bw.Kenani Kihongosi akiongoza vijana kwenye matembezi kutoka katika Uwanja wa Benjamini Mkapa mpaka kwenye viwanja vya Muembe Yanga Temeke Jijini Dar es salaam katika uzinduzi wa Uhamasishaji wa SENSA ya Watu na Makazi ambayo itakuwa endelevu kwa nchi nzima.SENSA ya Watu na Makazi inatarajia kufanyika Agosti 23,2022. Maelfu ya vijana wakitanzania wakiwa kwenye matembezi ambayo yameanzia katika Uwanja wa Benjamini Mkapa mpaka kwenye viwanja vya Muembe Yanga Temeke Jijini Dar es salaam katika uzinduzi wa Uhamasishaji wa SENSA ya Watu na Makaziambayo itakuwa endelevu kwa nchi nzima.SENSA ya Watu na Makazi inatarajia kufanyika Agosti 23,2022.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

****************************

Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa, Bw.Kenani Kihongosi leo Juni 23,2022 ameongoza maelfu ya vijana kwenye matembezi kutoka katika Uwanja wa Benjamini Mkapa mpaka kwenye viwanja vya Muembe Yanga Temeke Jijini Dar es salaam katika uzinduzi wa Uhamasishaji wa SENSA ya Watu na Makazi ambayo itakuwa endelevu kwa nchi nzima.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Kihongosi amesema sensa ni msingi wa maendeleo lakini sensa inachochea maendeleo, Serikali inapokwenda kutambua watu wake ni dhahiri kwamba itapeleka kulingana na idadi ya watu wake.

"Tumeona baadhi ya maeneo kumekuwa na changamoto, kwanza watu walipohesabiwa mwaka 2012 ,wengine hawakuhesabiwa ,sasa Serikali inapopeleka fedha kama inalenga hospitali ,ujenzi wa shule, kuboresha huduma inapeleka kwa idadi ya namba ambayo imeandikishwa ,kumbe idadi ya watu ni kubwa ,sisi Umoja wa Vijana wajibu wetu mkubwa ni kuhakikisha tunaungana na Serikali na kuwaleza Watanzania wote wakiwemo vijana wenzetu kwamba sensa ni kitu muhimu na tunaisadia Serikali katika kusukuma ajenda ya maendeleo". Amesema Bw.Kihongosi.

Amesisitiza vijana wajitokeze kwa wingi lakini waende kuhamasisha wenzao kwasababu siku ya leo wamekuwa na vijana ambao wanatoa elimu juu ya sensa,ambapo wanawakufunzi wa sensa kutoka serikalini lakini wapo watu ambao wametunga nyimbo zinazohamasisha sensa na kueleza umuhimu wa sensa .

"Kwa hilo ni jambo la pili na jambo la tatu kampeni hii itakuwa endelevu hapa Dar es Salaam na kampeni tumezindua leo tarehe 23 mwezi wa Sita lakini tutakwenda katika mikoa yote ya Kanda ya ziwa, tutakwenda Kanda ya kaskazini , tutakwenda Kusini,lengo ni kuwakumbusha Watanzania na wajue sensa ina umuhimu mkubwa katika maendeleo lakini pia tutafika mpaka Zanzibar na kama ambavyo unafahamu Taifa letu ni Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tumeungana Tanzania Bara na Tanzania Visiwani kwa hiyo tunawajibu kufika mpaka Zanzibar kwenda kuhamasisha vijana na Watanzania kuhusiana na suala Zima la sensa.". Amessisitiza Bw.Kihongosi.

Aidha amesema katika elimu ya sensa kama kuna Wizara ambayo inahusika na masuala ya kuratibu sensa ndio maana wameleta watalaam kutoka serikalini ambao watagusa maeneo yote yanayohitajika kuhusu sensa ,waeleza kwanini kuna sensa na inahesabiwa kwa Watanzania na kwanini pia Wananchi wahesabiwe maana Watanzania wataenda kufahamu kumbe wakihesabiwa.

Post a Comment

0 Comments