Ticker

6/recent/ticker-posts

KONGAMANO LA MASUALA YA UTAFITI KATIKA HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI-MLOGANZILA

Mkurugenzi wa Taasisi ya magonjwa ya Binadamu (NIMR) Prof.Yunus Mgaya akizungumza katika kongamano la masuala ya utafiti Lililofanyika katika Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila leo Juni 15,2022 Jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Prof.Lawrence Museru akizungumza katika kongamano la masuala ya utafiti Lililofanyika katika Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila leo Juni 15,2022 Jijini Dar es Salaam. Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili-Mloganzila Dkt.Julietth Magandi akizungumza katika kongamano la masuala ya utafiti Lililofanyika katika Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila leo Juni 15,2022 Jijini Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Kamati ya Utafiti -Mloganzila Dkt.Lulu Sakafu akizungumza katika kongamano la masuala ya utafiti Lililofanyika katika Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila leo Juni 15,2022 Jijini Dar es Salaam.Mwakilishi wa taasisi ya Kikorea inayojishugulisha na masuala ya tafiti na Sayansi Bw.Kimson Park akizungumza katika kongamano la masuala ya utafiti Lililofanyika katika Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila leo Juni 15,2022 Jijini Dar es Salaam.Mkurugenzi wa Taasisi ya magonjwa ya Binadamu (NIMR) Prof.Yunus Mgaya akielekezana jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Prof.Lawrence Museru katika kongamano la masuala ya utafiti Lililofanyika katika Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila leo Juni 15,2022 Jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Taasisi ya magonjwa ya Binadamu (NIMR) Prof.Yunus Mgaya akimsikiliza mmoja wa watafiti katika kongamano la masuala ya utafiti Lililofanyika katika Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila leo Juni 15,2022 Jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Taasisi ya magonjwa ya Binadamu (NIMR) Prof.Yunus Mgaya (katikati) akipata picha ya pamoja na wadau wa utafiti wa magonjwa mbalimbali katika kongamano la masuala ya utafiti Lililofanyika katika Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila leo Juni 15,2022 Jijini Dar es Salaam..

Baadhi ya wadau wa utafiti wakiwa katika kongamano la masuala ya utafiti Lililofanyika katika Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila leo Juni 15,2022 Jijini Dar es Salaam.

******************************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Mkurugenzi wa Taasisi ya Tafiti na Uchunguzi ya Magonjwa ya Binadamu (NIMR) Prof.Yunus Mgaya leo Juni 15, 2022 amefungua kongamano la masuala ya utafiti lililofanyika katika Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila leo Juni 15,2022 Jijini Dar es Salaam.

Akifungua Kongamano hilo, Prof. Mgaya amesema kuna haja ya kufanya utafiti kuhusu madhara madogo ya Covid 19 kwa Afrika na tayari upo utafiti uliofanyika lakini pia kuna Dawa tatu ambazo zimewekwa kwenye utafiti za Covid 19 ili kujua kama inatibi au kuleta unafuu.

Amesema kuwa kuna Hospital kubwa zilizopo hapa nchini zilionesha nia kwani tiba asili zinachukuliwa kama haina Tafiti hivyo wameshirikiana kutengenezwa utafiti wa pamoja wa tiba asili.

"Matokeo ya Tafiti ni kuwapa serikali wazitumie kuiboresha sekta ya Afya na pia kusambaza matokeo ya Tafiti kwa wananchi na tunasisitiza ushirikiano na Hospital kubwa ili kufanya tafiti tunawajengea uwezo wataalamu wa afya ,"Amesema

Kwa upande wake Mkurugenzi mkuu wa Hospital ya Taifa ya Muhimbili,Prof. Laurence Museru amesema ili kuiboresha mazingira ya utafiti Hospitali inatoa kiasi cha Sh. Milioni 10 kwa Kila Tafiti moja.

"Hospital inatenga hela wataalamu wakiomba na wakikidhi vigezo wanapewa zisaidie katika Tafiti, Tunashirikiana na NIMR watusaidie kugharamia Tafiti ambazo tunafanya ili ziweze kuleta matokeo mazuri". Amesema Prof.Museru.

Nae Mmoja wa watafiti ambaye amefanya utafiti wake katika Mkoa kilimanjaro juu ya hali ya usikivu kwa watoto wa shule ya msingi amesema katika utafiti wao wamebaini tatizo kubwa la usikivu kwa watoto ambalo limekuwa likipelekea watoto hao kufanya vibaya katika masomo.

Post a Comment

0 Comments