Ticker

6/recent/ticker-posts

UWT NJOMBE WAPONGEZA MAPENDEKEZO YA KUFUTWA ADA KWA WANAFUNZI KIDATO CHA TANO NA SITA


************************

MAPENDEKEZO ya kufutwa ada kwa wanafunzi wa kidato cha tano na sita yaliyotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan na kusomwa Bungeni na Waziri wa Fedha Dk Mwigulu Nchemba yamepongezwa Kwa nguvu zote na Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi(UWT)Mkoa wa Njombe.

Umoja huo kupitia kwa Mwenyekiti wa Mkoa huo Scholastika Kevela kimetoa pongezi hizo saa chache mara baada ya Waziri Nchemba kusoma mependekezo ya Bajeti ya Serikali ya Mwaka 2022-2023 ambayo pamoja mambo mengine imependekeza kufutwa kwa ada hiyo Kwa wanafunzi wa vidato hivyo.

Hatua hiyo muendelezo wa mambo mbalimbali makubwa yanayoendelea kufanywa chini ya uongozi wa Raise Samia Suluhu Hassan tangu aapishwe kwa mujibu wa katiba kuwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania zaidi ya Mwaka mmoja uliopita.

Akizungumza kuhusu hilo, Mama Kevela amesisitiza kwa kusema UWT Mkoa wa Njombe hauna chochote cha kumpa Rais Samia zaidi ya kumshukuru kwa hatua hiyo ambayo inakwenda kuyafuta kabisa machozi ya watazania wengi hususani wanyonge wenye vipato vya chini hapa nchini.

" UWT Mkoa wa Njombe tunazidi na tutazidi kuendelea kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa hatua nyingi anazozizifanya kuwapunguzia mzigo watanzania , amefuta vilio vya masikini wengi waliokuwa wahihi kutafuta hela kuwalipia watoto wao ada" alisema Kevela

Amesisitiza kuwa baada ya hatua ya aliyekuwa Rais mstaafu wa awamu ya Tano marehemu Dk John Magufuli kufuta ada kwa wanafunzi kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne, Rais Samia ' ameupiga mwingi' kwa pendekezo lake la kufuta ada kwa kidato cha tano na sita

Awali akisoma mapendekezo ya bajeti ya Serikali ya Mwaka 2022-2023 Bungeni Waziri wa Fedha Dk Mwigulu Nchemba alisema katika utekelezaji wa bajeti hiyo, Rais Samia alitoa mapendekezo ya kuondolewa kwa ada hiyo hatua ambayo kila mtanzani ameipokea kwa furaha.

" Kwa hilo hakuna ubishi, ni hapa juzi tu katoka kuwaondolea wafanyabiashara mzigo wa malimbikizo ya Kodi pamoja na ushuhuru mbalimbali wa zaidi ya miaka mitano iliyopita, alipandisha kima cha mishahara katika sekta ya umma nchini ili alilolifanya leo ni zaidi ya upendo kwa wananchi wake" alisisitiza Kevela

Alisema hatua hiyo ameonyesha kulijali Taifa analoliongoza kwani amewatua mzigo mzigo mzito wananchi wake hali iliyopelekea elimu nchini kuwa bure kuanzia elimu ya awali hadi kidato cha sita jambo ambalo halijawahi kutokea tangia uhuru.

"Watanzania watake nini zaidi ya Rais Samia Suluhu Hassan, kwa niaba ya wananchi wa mkoa wa Njombe nikiwa Mwenyekiti wao UWT niwatake wanawake wenzangu waliopo kila kona ya Tanzania kujitokeza na kuzitangaza kazi nzuri anazozifanya Rais Samia " alisisitiza Scholastika Kevela

Pamoja na rai yake hiyo kwa wanawake hao Mwenyekiti huyo wa UWT Mkoa wa Niombe pia aliwataka wanamme wote nchini kulichukulia suala hilo kwa uzito mkubwa kwani kitendo alichokifanya Rais kuondoa ada hiyo kinawapunguzia mzigo wa kusomesha watoto waliokuwa nao.

Alisisitiza Kwa kusema watanzania wote wamelipokea suala hilo kwa mikono miwili na zaidi ana amino kuwa wakati wote wataendelea kumuunga mkono huku akiwataka kumuombea Dua njema kwa Mungu apate kuwa na afya njema wakati wote ili azidi kuwatumikia.

Post a Comment

0 Comments