Ticker

6/recent/ticker-posts

TAMASHA LA ZIFF KUFUNGULIWA JUNI 18 MATAIFA 33 KUSHIRIKI

Mratibu wa Tamasha la ZIFF Prof. Martini Muhando akizungumza jijini Dar es Salaam na Wasanii wa Bongo Movie, wadau na mabalozi wa nchi ambao filamu zao zimebahatika mwaka huu kushiriki.
Balozi wa Ujermani Nchini Tanzania Regina Hess akizungumza Dar es Salaam na Wasanii wa Bongo Movie, wadau na mabalozi wa nchi ambao filamu zao zimebahatika mwaka huu kushiriki.Baadhi ya wadau wa Tamasha la ZIFF wanaotarajiwa kushiriki


*****************************

NA MAGRETHY KATENGU, DAR ES SALAAM

TAMASHA la Kimataifa la Filamu Zanzibar International (ZIFF) latarajiwa kufunguliwa Juni 18 na kilele chake kuwa Juni 26 mwaka huu.

Hayo yamebainishwa jijini Dar es Salaam jana na Mratibu wa Tamasha hilo Prof. Martini Muhando akizungumza na Wasanii wa Bongo Movie, wadau mbalimbali ikiwemo mabalozi wa Nchi ambao filamu zao zimebahatika mwaka huu kushiriki.

“Tarehe 18 ndiyo itakuwa siku ya kufungua tamasha, na katika siku hiyo ya tamasha tutakuwa na filamu moja ambayo itakuwa inaonyeshwa ni filamu ambayo imevunja rekodi zote hapa Tanzania kwa filamu ambayo ilipendwa sana na sasa hivi inatembea nchi nzima. Filamu yetu ya kufungua tamasha letu mwaka huu ni ‘Vuta ni kuvute’,”wote mnaifahamu itatuinua kidedea kuongoza Duniani alisema Prof. Muhando na kuongeza,

Hata hivyo Prof. Muhando aliwapongeza kina Dkt. Issa Shivji kwa kufanya filamu hiyo ambayo anaamini itakuwa bora katika Tanzania kwani ni nzuri na yakipekee kufanyika katika zama hizi.

“Nia yetu ni kwamba katika miaka hii ya kuanzia 2015 mpaka 2024, kwa miaka hii 10 ni miaka ya kusherehekea mchango wa watu weusi katika maendeleo ya Dunia, sasa Tanzania bado haijafanya chochote katika hilo, lakini sisi tukachukua nafasi hii ya kusema kwamba tunataka tuonyeshe ulimwengu kwamba sisi Waafrika historia yetu kwanza tunajivunia historia yetu, lakini vile vile tuko tayari kuchangia zaidi kwenye maendeleo ya Dunia,” alisema Prof. Muhando na kuongeza,

“Kwahiyo siku ya tarehe 18 usiku wataondoka watu wakitokea 15 wakitokea Bagamoyo kuelekea Zanzibar, tutawapokea pale tarehe 19 asubuhi, wale wageni wetu ni wageni mchanganyiko Watanzania wazawa pamoja na Wamarekani Weusi ambao walihamia Tanzania baada ya kuona kwamba wametambua Afrika kama nyumbani kwao. Kwahiyo sisi tutawapokea pale kama watu huru,”.

Sanjari na hayo alisema mwaka jana kwa mara ya kwanza Serikali ya Marekani ilitambua kwamba hiyo ni siku muhimu sana kwa watu weusi au kwa maana ya wenye asili ya Afrika waishio Marekani kwamba siku hiyo kila mwaka watakuwa wakifanya sherehe kwa sababu wanatambua historia kati ya Zanzibar na watu waliopelekwa utumwani wameamua kwamba watasherehekea siku hiyo visiwani Zanzibar.

Alibainisha kuwa tamasha hilo litakuwa na jumla ya filamu 101 ambazo zinatoka nchi 33 kwamba hii inaonesha ni namna gani tamasha hilo ni la kimataifa.

Naye Balozi wa Umoja wa Ulaya Nchi Tanzania Manfredo Faut amesema Utamaduni na Sanaa ni kitu cha muhimu kinatangaza Taifa na kinatengeneza fursa mbalimbali za ajira kiuchumi hivyo vijana wasibweteke wajitokeze kukuza vipaji vya walivyo navyo

Pia Balozi wa Ufaransa Nabil Hjloui ameeleza kuwa wako tayari kushirikiana na Tanzania kuhakikisha wanazalisha Filamu bora kwa kutumia Teknolojia ya kisasa ili waendane na soko la Kimataifa

Kwa upande wake Balozi wa Ujerumani Nchini Regina Hess amesema Tanzania na Ujerumani wana ushirikiano wa muda mrefu na kuna baadhi ya vitu vya kihistoria vipo Tanzania na baadhi ya wananchi wao huja kutembelea kufanya Utalii hivyo Tamasha hilo wanaopenda liwe endelevu kuwasaidia vijana kupata ajira

Aidha watu wote wadau wanakaribishwa kushiriki katika tamasha na kutoa ushirikiano Kwa namna yeyote hivyo linalotarajiwa kuzinduliwa June 18 Mwaka huu Zanzibari na kuhudhuria na Mataifa 33 ikiwemo Irani,Afrika kusini,Kenya,

Post a Comment

0 Comments