Ticker

6/recent/ticker-posts

WAZIRI OMAR SHABANI AWASILISHA MSIMAMO WA SERIKALI YA TANZANIA WA KUUNGA MKONO MAAMUZI YA KUONDOA UZUIAJI WA CHAKULA KUTOKA NJE


***************

Leo tarehe 14/6/2022 Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda, Zanzibar Mhe. Omar Said Shabani amewasilisha msimamo wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa kuunga mkono maamuzi ya kuondoa uzuiaji wa Chakula Kutoka Nje ya Nchi kinachonunuliwa na shirika la World Food Programe (WFP )kwa sababu za kibinadamu.

Katika mkutano mkuu wa 12 wa nchi wa Shirika la Biashara Duniani (WTO) unaofanyika Geneva ,Uswisi ulioanza tarehe 12 Juni ,2022 unaohudhuriwa na wajumbe wengine kutoka Tanzania. Awali Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ilichelea kuunga mkono pendekezo hilo mpaka ilipojihakikishia kuwa uamuzi huo hautazuia nchi kuchukua hatua ya kuzuia ikiwa kuna tishio la usalama wa chakula.

Mkutano huo unatarajiwa kumalizika tarehe 15/6/2022.

Post a Comment

0 Comments