Ticker

6/recent/ticker-posts

TBS YAWATAKA WAJASIRIAMALI WA BIDHAA ZA USINDIKAJI WA VYAKULA KUTUMIA MAFUNZO WANAYOPEWA KUKUZA BIASHARA ZAO


Maafisa wa TBS wakimweleza mjasiriamali taratibu za kupata leseni ya kutumia alama ya ubora ya TBS sambamba na taratibu za kuzalisha bidhaa zenye ubora kama uzingatiaji wa usafi na mpangilio sahihi wa eneo.
Meneja wa Huduma za Maktaba na Taarifa, Bi. Bahati Samilani akiwaelekeza wateja jinsi kuangalia viwango kupitia tovuti ya TBS.

*************

Taasisi za Serikali, asasi na sekta binafsi na wajasiriamali wadogo wa bidhaa za usindakaji vyakula mbalimbali zikiwemo za mkonge, viungo na zinginezo wameshauriwa kuyapa kipaumbele mafunzo yanayotolewa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kwani yana faida kubwa katika suala zima la kukuza biashara nchini.

Ushauri huo umetolewa na Afisa Usalama wa Chakula wa TBS,William Mhina, wakati akizungumza kwa nyakati tofauti na washiriki pamoja na wananchi kwenye Monesho ya Biashara Tanga yaliyoandaliwa na TCCIA yaliyofanyika Viwanja vya Mwahako mkoani Tanga kuanzia Mei 28 hadi Juni Juni 6, mwaka huu.

Mhina aliwaambia washiriki na wananchi waliohudhuria maonesho hayo kwamba TBS ipo kwa ajili ya kusaidia uzalishaji wa bidhaa zenye viwango ili kuziwezesha kushindana kwenye masoko ya ndani na nje ya nchi bila vikwazo vya kibiashara. "TBS ni wadau wakubwa ukizingatia lengo mojawapo la kuanzishwa kwa shirika hili ni kuwezesha biashara.

Tumekuja kwenye maonesho haya ili kuwasogezea huduma wajasiriamali tuweze kujua changamoto zao sambamba na kuwapa elimu ya kuthibitisha ubora wa bidhaa zao hasa ukizingatia kwamba huduma hii inatolewa bure kwao," alisema Mhina na kuongeza;

"Serikali inatenga kati ya sh. milioni 150 hadi 200 kila mwaka kwa ajili ya kuwahudumia wajasiriamali, hivyo ni fursa nzuri kwao kujitokeza kuthibitisha ubora wa bidhaa zao bure ili waweze kuondokana na vikwazo vya kibiashara." Kwa mujibu wa Mhina hadi sasa sasa zaidi ya wajasiriamali wadogo 500 kutoka mikoa mbalimbali wamepata leseni chini ya mpango huo wa bure

Akizungumza kwenye maonesho hayo mjasiriamali, Ashura Omari anayezalisha mafuta ya alizeti wilayani Kilindi mkoani Tanga, alisema;

"Nilishaanza uzalishaji wa mafuta ya alizeti na kuna wakati sikufuata utatatibu nikafungiwa kwa sababu nilikuwa nazalisha bila kufuata taratibu sahihi za uzalishaji kwa kuogopa kufuatilia TBS, lakini sasa nimeelimika nimejua TBS hawakuwa na nia mbaya nimejipanga upya na kwa sasa nimefahamu utaratibu wa kufuata baada ya kuhudhuria semina za TBS," alisema Omari.

Aliwashauri wajasiriamali wenzake na wazalishaji wa bidhaa za aina mbalimbali kwa ujumla wasiikimbie TBS na badala yake wakisikia mafunzo yanayotolewa na Shirika hili wahudhurie kwa wingi kwa kuwa yana faida nyingi kwenye uzalishaji wao.

Alisema TBS wapo kwa nia ya kusaidia kutoa elimu na kuwezesha uzalishaji unaozingatia viwango.

TBS hutoa mafunzo kwa wazalishaji katika ngazi za mikoa na wilaya bila malipo yoyote kwa lengo la kukuza ulewa wa viwango na kuhakikisha uzalishali wa bidhaa zenye ubora unaongezeka.

Maonesho hayo yalifungwa jana na Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar,Mhe. Simai Mohamned Said, ambapo kauli mbiu ilikuwa na ujumbe usemao; "Ushirikiano na sekta ya umma na binafsi ndio injini ya maendeleo ya uchumi.

Post a Comment

0 Comments