Ticker

6/recent/ticker-posts

TIC NA NIDA ZASAINI MKATABA WA KUWAHUDUMIA WAWEKEZAJI KUPITIA MFUMO WA PAMOJA

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TIC Ndg. John Mnali (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi Usajili kutoka NIDA Ndugu Edson Guyai (kulia), kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu NIDA wakionesha nakala za mikataba ya mashirikiano ya huduma ya pamoja Kwa wawekezaji iliyosainiwa Leo na Tasisi hizo ili kuanza utekelezaji.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TIC Ndg. John Mnali (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi Usajili kutoka NIDA Ndugu Edson Guyai (kulia) Kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu NIDA, wamesaini mikataba ya ushirikiano ya huduma ya pamoja kwa wawekezaji katika ukumbi wa TIC uliopo Mtaa wa Shaban Robert jijini Dar es salaam
Mwakilishi wa Wizara ya Ardhi TIC Ndg. Jonas Chikawe akishuhudia utiaji saini wa mikataba ya mashirikiano ya Huduma ya pamoja kwa wawekezaji kati Wizara ya Ardhi na TIC uliofanywa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TIC Ndg. John Mnali kwenye ukumbi wa kituo cha uwekezaji Tanzania leo tarehe 10 June 2022.
Baadhi ya wafanyakazi wa TIC wakishuhudia utiaji Saini wa mikataba ya mashirikiano ya huduma ya pamoja Kwa Wawekezaji kati ya TIC na NIDA kwenye Ukumbi wa kituo cha uwekezaji Tanzania leo tarehe 10 June 2022.
Pichani ni wafanyakazi wa TIC na wafanyakazi kutoka Taasisi mbalimbali za Serikali waliohudhuria katika kusaini mikataba ya mashirikiano ya Huduma Kwa Wawekezaji iliyoongozwa na Kaimu Mkurugenzi mtendaji wa TIC Ndugu John Mnali  kwenye Ukumbi wa kituo Cha uwekezaji uliopo mtaa wa Shaban Robert jijini Dar es salaam
Baadhi Wakurugenzi na Viongozi mbalimbali kutoka Tasisi za serikali wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kukamilisha zoezi la utiaji saini wa mikataba ya mashirikiano ya huduma ya pamoja wa wawekezaji katika kituo cha uwekezaji Tanzania leo tarehe 10 June 2022..

*****


 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Ndg. John M. Mnali katika kuhakikisha maboresho ya huduma kwa wawekezaji hasa kwa kutumia mifumo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) unafanikiwa wamesaini makubaliano ya awali ya mashirikiano na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) ili kutumia mfumo wa pamoja ambao utawezesha huduma wanazotoa NIDA  na TIC kwa wawekezaji kuweza kusomana/kuonekana kwenye mfumo mmoja.

Hafla hilo fupi limefanyika  katika ukumbi wa mikutano wa TIC uliopo mtaa wa Shaban Robert jijini Dar es Salaam leo tarehe 10 Juni, 2022.

Taasisi 12 za Serikali zinazotoa huduma kwa wawekezaji  zimekubaliana kusaini mikataba ya mashirikiano ya awali ili  kutumia mfumo mmoja wa huduma Kwa wakezaji katika kuhakikisha Wawekezaji wanapata huduma zote Kwa urahisi na haraka. NIDA na TIC tayari wamesaini makubaliano hayo taasisi zingine ambazo bado zitakamilisha suala hilo kabla ya tarehe 15 Juni, 2022.

Kituo cha uwekezaji Tanzania  kinafanya kazi pamoja na taasisi kumi na mbili za Serikali zinazotoa huduma mahala pamoja (NIFC ) taasisi hizo ni BRELA, NEMC, NIDA, TRA, UHAMIAJI, ARDHI, KAMISHINA WA KAZI, TANESCO, OSHA, TBS na TMDA.

Post a Comment

0 Comments