Ticker

6/recent/ticker-posts

WAZIRI BASHUNGWA AIPONGEZA YANGA KWA KUTWAA KOMBE KWA BINGWA WA LIGI KUU


***********************

Na OR TAMISEMI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Innocent Bashungwa ameipongeza klabu ya Yanga kwa kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya mpira wa miguu (NBC Premiear League) msimu huu, 2021/2022 unaowapa fursa ya kushiriki mashindano makubwa ya kimataifa ya klabu bingwa Afrika.

Ametoa pongezi hizo Juni 25, 2022 Jijini Mbeya wakati akikabidhi kombe kwa bingwa wa ligi kuu msimu huu wa 2021/2022 baada ya mchezo kati ya klabu ya Mbeya city na klabu ya Yanga katika Uwanja mpira wa Sokoine.

Bashungwa baada ya kukabidhi kombe hilo, amempongeza Mheshimiwa Rais Samia Suluhu hassan kwa juhudi kubwa za kuendeleza sekta ya michezo hapa nchini kwa kasi ya kubwa na amekuwa akitoa miongozo, maelekezo, motisha na uwezeshaji mkubwa katika mchezo wa mpira wa miguu na sekta nzima.

ametoa wito kwa wanamichezo kuendelea kujituma kwa kuwa michezo ni Ajira, kwasababu wachezaji huibuliwa na kuanzia ngazi za chini, Ofisi ya Rais TAMISEMI itaendelea kushirikiana na Wizara yenye dhamana ya michezo na wadau wengine kuhakikisha sekta ya michezo inasonga mbele.

Aidha, Bashungwa amevitaka vyama na vilabu vya michezo kushiriki katika michezo ya UMITASHUMTA na UMISSETA ili kupata vipaji vya kuendeleza sekta hii na kwa mashindano hayo ngazi ya wilaya na mikoa.

Vile vile, amempongeza Waziri mwenye dhamana ya michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa kwa kwa kumsaidia Mheshimiwa Rais, ambapo ndani ya muda mfupi Tanzania imeweza kutwaa makombe na kufuzu kwa kombe la Dunia kwa Timu ya Taifa ya mpira wa miguu kwa watu wenye ulemavu (Tembo worriors) litakalochezwa nchini Uturuki na timu ya wanawake chini ya Umri wa miaka 17 (U17) Serengeti girls kule nchini India.

Post a Comment

0 Comments