Ticker

6/recent/ticker-posts

DKT. MAPANA AWAWEKA MGUU SAWA WASANII NCHINI KUELEKEA SENSA YA WATU NA MAKAZI AGOSTI 23


*************

Na Mwandishi Wetu Chamwino.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Dkt. Kedmon Mapana amewataka Wasanii na wadau wa Sanaa nchini kuwa tayari katika zoezi la kuhesabiwa la Sensa ya Watu na Makazi ambayo itafanyika tarehe 23 Agosti 2022, kote Bara na Visiwani Zanzibar.

Dkt.Mapana amebainisha hayo katika Tamasha la muziki wa Wagogo maarufu kama Cigogo Music festival ambalo mwaka huu ni la msimu wa 13, linalofanyika kwa siku mbili Julai 23-24, Kijiji cha Chamwino Ikulu.

Ambapo amewataka Wasanii kuwa mstari wa mbele, kuhesabiwa na hata kutunga nyimbo za kuhamasisha zoezi hilo la Sensa ya Watu na Makazi,

"Wasanii wote, kwa Sasa zoezi ni moja, kwenda kwenye Sensa ya Watu na Makazi, Agosti 23, mwaka huu. Tunaenda "kusensabika", sote kwa pamoja tujiandae kusensabika." Alisema Dkt.Mapana.

Aidha, Dkt. Mapana ametumia nafasi hiyo, kuwapongeza waandaji wa Tamasha hilo kwa mwaka huu, ambapo licha ya yeye awali kuwa mwanzilishi na Mwenyekiti wa Tamasha hilo kwa miaka iliyopita na kwa sasa kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan, kushika nafasi ya Katibu Mtendaji wa BASATA.

Tamasha hilo kwa mwaka huu lenye kauli mbiu, "Elimu ya Sanaa, ni muhimu kwa maendeleo endelevu", inashirikisha vikundi 32 huku kati yake vikundi 5 vikitoka mikoa ya Iringa, Njombe, Singida, Morogoro na Dar es Salaam na vilivyobakia Mkoa wa Dodoma,

Aidha, vikundi mbalimbali vimepata kuonesha Sanaa ya ngoma mbalimbali za kabila hilo la Wagogo, na makabila mengine waalikwa.

Post a Comment

0 Comments