Ticker

6/recent/ticker-posts

JAMII FORUMS YAZINDUA AWAMU YA PILI YA SHINDANO LA " STORIES OF CHANGE"

Mkurugenzi Mkuu wa JamiiForums, Bw.Maxence Melo akizungumza na waandishi wakati wa uzinduzi wa awamu ya pili ya shindano la 'Stories of Change' Katika Ofisi za Jamii Forums Jijini Dar es Salaam leo Jumatano Julai 13, 2022 Mhadhiri Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Shule Kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano kwa umma SJMC Bw. Abdalah Katunzi akizungumza na waandishi wakati wa uzinduzi wa awamu ya pili ya shindano la 'Stories of Change' Katika Ofisi za Jamii Forums Jijini Dar es Salaam leo Jumatano Julai 13, 2022 Mkurugenzi Mkuu wa JamiiForums, Bw. Maxence Melo akipata picha ya pamoja na Mhadhiri Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Shule Kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano kwa umma SJMC Bw. Abdalah Katunzi wakati wa uzinduzi wa awamu ya pili ya shindano la 'Stories of Change' Katika Ofisi za Jamii Forum's Jijini Dar es Salaam leo Jumatano Julai 13, 2022.

**********************

Katika kuhamasisha uandishi wa maudhui yenye tija mtandaoni na kuhakikisha mtandao unabaki mahali salama Asasi ya JamiiForums imezindua awamu ya pili ya shindano la " Stories of Change" litakaloanza Julai 15, 2022 na kumalizika Septemba 14, 2022.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam leo Julai 13,2022 Mkurugenzi Mkuu wa JamiiForums, Maxence Melo amesema uzinduzi wa awamu yapili unakuja kutokana na mafanikio yaliyopatikana katika awamu ya kwanza ya shindano hilo .

"JamiiForums ikishirikiana na Shule Kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano kwa umma , Chuo kikuu cha Dar es Salaam SJMC na Muungano wa Klabu za Waandishi wa habari ( UTPC) imeaandaa awamu ya pili ya shindano la" Stories of Change", amesema Maxence

Ameongeza kuwa shindano hilo linalenga kuongeza maudhui bora hususani ya lugha ya Kiswahili kwa ajili ya vizazi vya sasa na baadae.

" Shindano linalenga kuhamasisha ushiriki wa raia yakiwemo makundi yasiyopewa vipaumbele kama watu wanaoishi na ulemavu kushiriki katika ukusanyaji na utayarishaji wa taarifa nchini", amesema .

Kuhusu vigezo na masharti ya kushiriki katika shindano hilo Maxence amebainisha kuwa mshiriki anatakiwa kutayarisha andiko linalochochea mabadiliko kwenye nyanja za Elimu, Biashara/ Uchumi , Afya, Utawala Bora, Demokrasia , Kilimo, Sayansi na Teknolojia ambalo litaandikwa kwa lugha ya Kiswahili lenye maneno yasiyozidi 800-1000 na kuliweka andiko lake katika Jukwaa la Jamii Forums.

Akizungumzia zawadi kwa washindi amesema mshindi wa Kwanza atapata fedha taslimu shilingi Milioni 5 , Mshindi wa Pili Milioni 3, wa tatu Milioni 2, wa 4 Milioni 1 na watano ni shilingi laki 5 huku mshindi wa sita mpaka kumi watapata Shilingi laki tatu kila mmoja na mshindi wa kumi mpaka Ishirini watapata Shilingi laki moja kila mmoja.

Amesema washindi watapatikana kwa kuzingatia kura zitakazopigwa kwenye mnakasha ( thread) husika (30%) na pia uamuzi wa jopo la majaji (70%)

Post a Comment

0 Comments