Ticker

6/recent/ticker-posts

NIT YARIDHISHWA NA KASI YA WANAFUNZI KUENDELEA KUJIDAHILI CHUONI HAPO


*****************

CHUO Cha Taifa Cha Usafirishaji (NIT) kimeridhishwa na kasi ya wanafunzi kuendelea kujidahili na chuo hicho na kuwataka watu wote wenye malengo ya kufanya kazi katika miradi ya kimkakati kujiunga na masomo chuoni hapo.

Hayo yamebainishwa na Afisa Uhusiano Mkuu wa chuo hicho Tulizo Chusi wakati wa kuhitimishwa Kwa maonyesho ya 17 ya Vyuo Vikuu yaliyoandaliwa na Time ya Vyuo Vikuu nchini(TCU) Jijini Dar es Salaam.

Amesema kupitia maonyesho hayo NIT imefanikiwa kudahili wanafunzi kwa zaidi ya asilimia ya lengo iliyokuwa imejiwekea hatua iliyowafanya waone kuwa chuo hicho kinaendelea kukubarika na watu kutoka maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi.

"Maonyesho yamewapa fursa watu wengi kufahamu undani wa masomo yanayofundishwa chuoni kwetu, tunazidi kuwasisitiza wale wote wenye malengo ya kufanya kazi katika miradi mbalimbali ya kimkakati hapo baadae kujiunga na NIT" amesema Tulizo

Aidha aliwapongeza TCU kwa kuandaa maonyesho hayo kwa kuwa mbali na kutoa fursa ya wanafunzi kufanya udahili wa moja kwa moja, pia yameviwezesha vyuo kujitangaza na hivyo kuwafanya wanafunzi kuelewa undani wa masomo wayapendayo.

Manyesho hayo yaliyovishirikisha vyuo zaidi ya 75, yalianza jumatatu iliyopita na kufunguliwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, yalihitimishwa rasmi jumamosi iliyopita na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Francis Michael kwa niaba ya Waziri Profesa Adolf Mkenda.

Akizungumza wakati akifunga maonyesho hayo, Katibu Mkuu huyo amesema Serikali inaendelea kufanya maboresho katika elimu ya vyuo vikuu nchini ambapo katika mwaka huu zaidi ya mitaala 300 inafanyiwa mapitio ikihusishwa na maoni mbalimbali ya wadau.

Aidha kwa nyakati tofauti Mkuu wa Chuo Cha Taifa Cha Usafirishaji(NIT) Profesa Zacharia Mganilwa amesema ili kuongeza ufanisi na kuisaidia sekta ya usafirishaji chuo hicho kimeendela kutoa mafunzo mbalimbali ya nadharia na vitendo kwa lengo la kutimiza adhma ya Serikali.

Amesema kufikia adhma hiyo hususani ya kuwaandaa wataalam wa kufanya kazi katika miradi mbalimbali ya kimkakati, NIT imeanzisha masomo yanayolenga kukidhi matakwa hayo na kuwataka wazazi na wananchi kwa ujumla kukitumia chuo hicho kikamilifu.

Post a Comment

0 Comments