Ticker

6/recent/ticker-posts

TBS YAWATAKA WAAGIZAJI NA WAZALISHAJI WA BIDHAA ZA MABATI NA NONDO KUZINGATIA VIGEZO VYA UBORA

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Bw.david Ndibalema akizungumza katika ufunguzi wa kikao cha waagizaji, Wazalishaji na wasambazaji wa bidhaa za mabati, koili za mabati na nondo nchini uliofanyika leo Julai 22,2022 katika ofisi za TBS Jijini Dar es Salaam Baadhi ya wazalishaji na wasambazaji wa bidhaa za mabati na nondo nchini wakiwa kwenye kikao na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) uliofanyika leo Julai 22,2022 katika ofisi za TBS Jijini Dar es Salaam

********************

SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) litaendelea kuimarisha ukaguzi wa bidhaa za mabati na nondo zinazofika nchini na zikiwa katika soko ili kujiridhisha juu ya ubora wake na kuchukua hatua stahiki kwa mujibu wa sheria.

Ameyasema hayo leo Julai 22,2022 Jijini Dar es Salaam Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Bw.david Ndibalema wakati wa ufunguzi wa kikao cha waagizaji, Wazalishaji na wasambazaji wa bidhaa za mabati, koili za mabati na nondo nchini.

Amesema lengo la Mkutano huu ni kukuza uelewa wa wadau ili kukidhi matakwa ya Viwango kwa bidhaa za Mabati, Nondo na Koili za kutengeneza Mabati hapa nchini.

"TBS inawajibika kikamilifu kuhakikisha kuwa bidhaa zinazozalishwa nchini na zile zinazoingizwa kutoka nje ya nchi ikiwa ni pamoja na bidhaa za Mabati, Koili za kutengeneza Mabati na Nondo zinakidhi matakwa ya Viwango ili kukuza uchumi wa Nchi yetu" - Amesema Bw.Ndibalema

Aidha amesema azma ya Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ni kujenga uchumi imara na endelevu, wenye Nguvu na ushindani hivyo ni jukumu letu TBS kuhakikisha bidhaa zinazozalishwa zinakidhi vigezo na ubora.

"Mada zitakazotolewa hapa na Wataalam wetu kutoka TBS zitahusu matakwa ya Viwango ambavyo ni TZS 353:2020/EAS. 11:2019 na TZS 1477:2020/EAS. 468:2019 Kwa bidhaa za Mabati na Koili vilivyoainishwa katika ngazi ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kupitishwa kuwa Viwango vya Kitaifa pamoja na kiwango Na. TZS 1476: 2017, Kwa ajili ya Nondo kiwango Na. TZS 142-1:2015 (3rd Ed) ISO 6935-1: 2007 na TZS 142-2:2015 (3rd Ed) ISO 6935-2:2007" - Amesema

Pia mada zingine zitakazotolewa ni kuhusu taratibu za uingizaji Nchini na Ukaguzi wa Shehena za Mabati na Koili na Nondo kutoka nje ya nchi.

" Nivyema kufahamu kwamba Viwango huandaliwa kupitia kamati zetu za kitaalam ambazo zimeundwa na Wadau mbalimbali ikiwemo nyinyi Wazalishaji pamoja na mfumo wa jumla wa utoaji maoni ambapo wadau mnahusishwa Moja kwa Moja kwa mantiki hiyo Viwango vitakavyofafaanuliwa katika kikao hiki vimepitia utaratibu huo" - Bw. David Ndibalema Kaimu Mkurugenzi Mkuu TBS

Post a Comment

0 Comments