Ticker

6/recent/ticker-posts

WAMILIKI WA MAGARI WAAGIZWA KUWAPA MIKATABA MADEREVA AGOSTI MWAKA HUU


Naibu Waziri Ofisi Waziri Mkuu Ajira,Kazi na Watu wenye Ulemavu Pratrobasi Katambi akizungumza katika kikao kazi kilichohusisha wajumbe kutoka sekta mbalimbali ikiwemo Wizara hiyo,mara baada ya kujadili malalamiko yaliyowasilishwa na vyama vya wafanyakazi madereva na Wamiliki wa Vyombo vya Usafiri..

************************

Na Magrethy Katengu

Serikali imewataka Waajiri wa vyombo vya Usafirishaji ikiwemo magari yanayosafirisha abiria na Mizigo kuwapatia mikataba ya kazi madereva kabla ya mwezi agosti mwaka huu na yeyote atakayekiuka agizo hilo hatu kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake .

Agizo hilo limetolewa Leo Dar es salaam na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Ajira,Kazi,Vijana na Watu wenye Ulemavu Patrobasi Katambi katika kikao kazi kilichohusisha wajumbe kutoka sekta mbalimbali ikiwemo Wizara hiyo,mara baada ya kujadili malalamiko yaliyowasilishwa na vyama vya wafanyakazi madereva na Wamiliki wa Vyombo vya Usafiri.

Sanjari na hayo amesema Serikali baada ya kupokea malalamiko hayo kutoka vyama vya wafanyakazi madera Ili kujiridhisha ilifanya ufuatiliaji nakubaini Jumla ya Makampuni 73 hayajazingatia takwa la kisheria la kuwapatia mikataba wafanyakazi hivyo amewataka wamiliki kuwapa mikataba wafanyakazi wao mara moja Ili kupungiza migogoro na migomo inayotokea mara kwa mara

Sambamba na hayo ameendelea kusema kwamba serikali pia imeweka utaratibu Kwa wamiliki wa magari yanayosafirisha mafuta na gesi nje ya nchi ikiwemo Nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Kongo kuwalipa posho kwa kuzingatia utaratibu wa kisheria wa malipo ya siku 20 za kusubiria kushusha na kupakia mzigo kwa dola 10 za kimarekani Kwa siku sawa na shilingi za kitanzania elfu 23000.

"Serikali kwa kuzingatia umuhimu wa posho hizi kwa madereva imeshirikisha vyombo vya utatu vinavyohusika kisheria kuishauri Serikali katika suala hili ambavyo ni LESCO na Bodi ya Kima cha Chini cha Mshabara kwa sekta Binafsi na kupokea maoni yao,Maoni hayo ambayo nimeyaridhia ni kiwango cha malipo ya safari ya kwenda na kurudi na mzigo(retuns )kuwa shilingi 330,000 na malipo ya kushusha na kupakua mzigo kuwa dola 170 za kimarekani" amesema Katambi.

Hata hivyo aliongezaa na "Nasisitiza viwango hivi vya posho ni sehemu ya mkataba wa hali bora kwa Wafanyakazi Madereva ambavyo vitapaswa kuzingatiwa na waajiri katika Mikataba ya ajira za Madereva.

WAZIRI Katambi amesema kuwa serikali itaendelea kufanya kaguzi za kazi ikiwa ni pamoja na kukagua mikataba hiyo kama imezingatia Makubaliano hayo,nakwamba kuhusu utaratibu wa kupakia na kushusha mafuta na gesi, Serikali imetoa Mwongozo wa kupakia na kushusha mafuta wa mwaka 2021 kwa wadau wote wa usafirishaji wa mafuta.

"Ni jukumu la kila Mdau kuhakikisha taratibu za upakiaji mafuta zinafuatwa wakati akiwa katika bohari yoyote,serikali itaendelea kutoa elimu kwa wadau wote ili waweze kuzingatia Mwongozo huu na hatua za kisheria zitachukuliwa kwa wadau watakaokiuka." Amesema Katambi

Waziri Katambi amesema Kuhusu mabasi ya abiria kuingia kila kituo kwa safari za mikoani. Serikali imeondoa vituo vilivyokuwa vinalalamikiwa ambapo kwa sasa magari hayalazimiki kuingia katika kila kituo, badala yake mabasi yataingia katika vituo vikuu hivyo LATRA imeshatoa ratiba mpya kutekeleza suala hili.

"Pamoja na hatua zilizochukuliwa, ninawasihi Viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi wazingatie utaratibu uliowekwa kisheria katika majadiliano ya kutetea maslahi ya wafanyakazi na kutatua migogoro ya kikazi. Aidha, nitoe rai kwa Madereva wasio wanachama wa Vyama vya Wafanyakazi kuacha kutumia njia zisizo halali kisheria kuanzisha au kuchochea vurugu na migomo"amesema Waziri Katambi

Aidha kuhusu usafirishaji sumu Kwa mujibu wa Sheria ya Kemikali za Viwandani na Majumbani Sura 182 ambayo imetoa mamlaka kwa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kusimamia wasafirishaji kwa kuwasajili wamiliki wa vyombo vya usafirishaji na kutoa mafunzo kwa Madereva wanaosafirisha sumu ndani na nje ya nchi.

Post a Comment

0 Comments