Ticker

6/recent/ticker-posts

UNESCO KUTOA MAFUNZO KWA WAWEZESHAJI WA MAFUNZO YA WALIMU KUHUSU ELIMU YA KUHUSIANA KWA HESHIMA, AFYA YA UZAZI, VVU/UKIMWI NA JINSIA.

Mgeni Rasmi wa ufunguzi wa mafunzo , Mhashama Baba Askofu Flavian Kassala, Makamu wa Rais wa baraza la maaskofu wa Tanzania na mwenyekiti wa Idara ya elimu, Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC). Muwakilishi wa UNESCO Tanzania Bw. Michel Toto akizungumza katika mafunzo kwa wawezeshaji wa mafunzo ya Walimu yanayolenga kutoa elimu ya stadi za maisha kuhusu kuhusiana kwa heshima, afya ya uzazi, VVU/UKIMWI na Jinsia.Mafunzo yameanza leo Julai 20,2022 Jijini Dodoma. Sehemu ya wawezeshaji wa TEC kwenye mafunzo.

************************

Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni UNESCO, kwa kupitia programu yake ya “Our rights,Our Lives, Our future” Inayofahamika kama O3 kutoa mafunzo kwa wawezeshaji wa mafunzo ya Walimu yanayolenga kutoa elimu ya stadi za maisha kuhusu kuhusiana kwa heshima, afya ya uzazi, VVU/UKIMWI na Jinsia.

Mafunzo haya yanatolewa kwa washiriki 54 kutoka katika dayosisi 18 za kanisa katoliki Tanzania jijini Dodoma, kuanzia leo tarehe 20 hadi 29 Julai 2022, yenye lengo la kusaidia wawezeshaji wa mafunzo ya walimu kuweza kufundisha walimu wa shule za msingi na sekondari katika dayosisi wanazotoka kuhusu kuhusiana kwa heshima,Afya ya Uzazi, VVU/UKIMWI na Jinsia. Mafunzo haya yatanufaisha walimu 1400 wa shule zaidi ya 700 za msingi na sekondari zilizopo katika dayosisi zote za kanisa katoliki Tanzania.

UNESCO kwa kushirikiana na Serikali kupitia wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Ofisi ya raisi tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI), Wizara ya afya, Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) na wadau wa elimu mbalimbali inachangia jitihada za serikali katika kuboresha mazingira salama ya kujifunzia kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari,ikiwemo kupata elimu sahihi ya afya ya uzazi inayozingatia umri, mila na desturi, kuzuia ukatili wa kijinsia, elimu ya VVU/UKIMWI na Kuhusiana kwa heshima.

Mafunzo haya ni sehemu ya mpango wa ushirikiano kati ya UNESCO, Taasisi ya Elimu Tanzania na Kanisa katoliki unaolenga kuboresha mazingira salama ya kujifunza na kufundishia shuleni kupitia kuwajengea uwezo walimu (utoaji mafunzo) na kusambaza miongozo inayohusu utoaji wa elimu husika.

Mpango huu unaotekelezwa kuanzia sasa hadi Desemba 2022 unategemea kuwajengea Walimu uwezo wa kufundisha mada husika na kuwajengea uwezo wanafunzi umahiri katika kujikinga na tabia hatarishi ikiwemo mimba za utotoni, unyanyasaji wa kijinsia, utumiaji wa mihandarati kwenye shule zilizo chini ya kanisa katoliki kupitia utoaji wa mafunzo na vitabu vya ziada kuhusu mada husika.

Post a Comment

0 Comments