Ticker

6/recent/ticker-posts

WAZIRI JAFO AZINDUA KAMPENI YA "BAHARI SAFI NI JUKUMU LANGU"

Mkuu wa Wilaya Kinondoni Mhe.Godwin Gondwe akifanya usafi katika fukwe za bahari Ramada jijini Dar es Salaam akiwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani jafo pamoja na wadau wa mazingira kwenye uzinduzi wa kampeni ya "Bahari Safi ni Jukumu langu". Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani jafo akiwa pamoja na wadau mbalimbali wa mazingira wakifanya usafi katika fukwe za bahari leo Julai 8,2022 Ramada Jijini Dar es Salaam kwenye uzinduzi wa kampeni ya "Bahari Safi ni Jukumu langu". Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani jafo akipanda mti kwenye fukwe za bahari Ramada Jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa kampeni ya "Bahari Safi ni Jukumu langu". Meneja Kanda ya Mashariki Kaskazini-NEMC Bw.Arnold Mapinduzi akizungumza katika uzinduzi wa kampeni ya "Bahari Safi ni Jukumu langu" ambapo aliungana Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani jafo pamoja na wadau mbalimbali wa mazingira kufanya usafi kwenye fukwe za bahari leo Julai 8,2022 Ramada Jijini Dar es Salaam. Balozi wa Mazingira, Bi.Winfrida Shonde akizungumza katika uzinduzi wa kampeni ya "Bahari Safi ni Jukumu langu" ambapo aliungana Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani jafo pamoja na wadau mbalimbali wa mazingira kufanya usafi kwenye fukwe za bahari leo Julai 8,2022 Ramada Jijini Dar es Salaam.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

**********************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani jafo ameliagiza Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kusimamia sheria ya mazingira kwa kuhakikisha wanatembelea hoteli zote ambazo wameshindwa kuendana na ajenda ya kimazingira na kuwachukulia hatua.

Waziri Jafo ameyasema hayo leo Julai 8,2022 wakati akizindua kampeni ya "Bahari Safi ni Jukumu langu" na kuungana na wadau wa mazingira pamoja na wananchi kufanya usafi katika eneo la Ramada Kunduchi Jijini dar es Salaam.

"NEMC hakikisheni mnawachukulia hatua wale wote ambao maeneo yao ya hoteli mazingira si masafi,na nipate ripoti ofisini kwangu ni hoteli ngapi zimeshindwa kucomply na mmezichukulia hatua". Amesema

Aidha Waziri Jafo amewataka wamiliki wa hoteli zilizopo kwenye ufukwe wa habari kuwa na wajibu wa kufanya usafi na kupanda miti maalumu ya fukwe ili kuhakikisha fukwe zinakuwa safi na salama kwa viumbe hai wa baharin.

Pamoja na hayo amewaagiza wenye viwanda kuhakikisha wanalinda mazingira katika eneo lao lote la kiwanda kuanzia mbele ya kiwanda hadi kwenda kwenye barabara ili Jiji liendelee kuwa safi na salama.

"Haiwezekani mtu anakiwanda kikubwa, amefanya uwekezaji lakini mbele ya kiwanda unakuta kuna makopo, kuna chupa pamoja na uchafu wa kila aina, anajukumu la kulinda mazingira kwa kuhakikisha mbele kuna kuwa safi na hata kwa kupanda miti mizuri na mji kuendelea kuwa safi". Amesema Waziri Jafo.

Kwa upande wake Meneja Kanda ya Mashariki Kaskazini-NEMC Bw.Arnold Mapinduzi amesema kila mtu anawajibu wa kutunza na kulinda mazingira na hii ni kutimiza haki ambayo mtanzania anatakiwa kuishi kwenye mazingira ambayo yapo safi na salama ili aweze kujilinda kutokana na mlipuko wa magonjwa mbalimbali

Hata hivyo amezitika taasisi mbalimbali nchini kuendelea kuhamasisha jamii katika utunzaji wa mazingira ili miji iendelee kuwa safi na salama na kuepuka milipuko ya magonjwa katika miji.

"NEMC tutaendelea kutoa ushirikiano wa kutosha kwa wadau mbalimbali wa mazingira ili juhudi na uhifadhi wa mazingira ziweze kuendelea hasa kupitia kampeni hii ya "Bahari Safi ni Jukumu langu" ambayo dhumuni lake ni kuhamasisha jamii kutunza na kulinda mazingira". Amesema Bw.Mapinduzi.

Post a Comment

0 Comments