Ticker

6/recent/ticker-posts

WAZIRI MKUU AKAGUA DARAJA LILILOJENGWA KWA TEKNOLOJIA MPYA YA MAWE MKALAMA SINGIDA

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akikagua Daraja la mawe lenye urefu wa mita 30 na upana wa mita saba lililojengwa katika Kijiji cha Lukomo barabara ya Iguguno-Kikhonda-Kinampundu wilayani Mkalama wakati wa ziara yake ya kikazi aliyoifanya leo wilayani humo mkoani Singida leo.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akifungua kitambaa kuashiria uzinduzi wa jengo la Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mkalama mkoani Singida ambalo limekamilika kwa asilimia 100. 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akikata utepe kuashiria uzinduzi wa jengo la Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mkalama mkoani Singida ambalo limekamilika kwa asilimia 100. 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisomewa taarifa na Meneja wa Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini Mkoa wa Singida Mhandisi Tembo David ya ujenzi wa Daraja la Mawe lililojengwa wilayani Mkalama.
Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Singida, Aysharose Mattembe akiwasalimia wananchi wa Kata ya Iguguno Kijiji cha Lukomo wakati wa ukaguzi wa daraja hilo.
Mbunge wa Iramba Mashariki, Francis Isack akizungumza kwenye ukaguzi huo.
Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Singida, Martha Gwau.akizungumza kwenye ukaguzi huo.

Ukaguzi wa daraja hilo ukiendelea.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwasalimia wananchi wa Kijiji cha Lukomo mara baada ya kuwasili kukagua daraja hilo.
Wananchi wa Kijiji cha Lukomo wakiwa kwnye ukaguzi huo.
Muonekano wa daraja hilo.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk.Binilith Mahenge wakati akisomewa taarifa ya ujenzi wa Daraja la Mawe lililojengwa wilayani Mkalama.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwapongeza Wahandisi wazawa waliojenga daraja hilo kwa kutumia gharama ndogo.
Mzee Rajabu Mbuga ni miongoni wa wananchi waliofika kumsikiliza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati wa ukaguzi wa daraja hilo.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama, James Mkwega (kulia) akiwa na Afisa Muuguzi wa wilaya hiyo, Ephrahim Kaphilimbi wakati wa ukaguzi wa daraja hilo.
Mkuu wa Wilaya ya Mkalama, Sophia Kizigo akiteta jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama, Asia Mesos wakati wa ukaguzi wa daraja hilo.
Wananchi wakionesha furaha zao baada ya daraja hilo kukamilika.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida, Alhajj Juma Killimbah akizungumza wakati waukaguzi wa daraja hilo.
Wananchi wakiwa wamesimama kwenye daraja hilo wakati wakimsikiliza Waziri Mkuu Kassi Majaliwa (hayupo pichani)
Ukaguzi wa daraja hilo ukiendelea.
Mwonekano wa jengo la Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mkalama.
Wananchi wakiwa kwenye hafla ya uzinduzi wa jengo la ofisi ya mkuu wa wilaya ya Mkalama.
Katibu Mwenezi wa CCM Mkoa wa Singida, Ahmed Kaburu na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) Mkoa wa Singida Jane Kessy wakiwa kwenye hafla ya uzinduzi wa jengo hilo.


**************************


Na Dotto Mwaibale, Mkalama, Singida

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amekagua daraja la mawe lililojengwa na Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (TARURA) Mkoa wa Singida  na kuokoa  Sh.448 milioni, daraja lililojengwa katika Kijiji cha Lukomo wilayani Mkalama kwa kutumia teknolojia mpya ya mawe.

Akizungumza kabla ya Waziri Mkuu hajalikagua daraja hilo Meneja wa TARURA Mkoa wa Singida, Tembo David, alisema kwa kutumia teknolojia mpya ya kulijenga kwa mawe limegharimu Sh.102 milioni.

" Daraja hili kama tungelijenga kwa njia ya kawaida lingeigharimu Serikali Sh.550 milioni lakini kwa kutumia teknolojia hii ambayo ni nafuu sana  inatumika nchini Hispania na hapa nchini madaraja kama hayo yamejengwa Mikoa ya Kigoma na Mbeya," alisema.

David alisema ujenzi wa daraja hilo lenye urefu wa mita 30 na upana wa mita 7 ulianza Disemba 18, 2021 na limekamilika Julai 18, 2022.

Meneja huyo aliishukru serikali kwa kuongeza bajeti ya ujenzi wa barabara katika Mkoa wa Singida kutoka Sh.6 bilioni hadi kufikia Sh.23.4 bilioni.

Waziri Mkuu, Majaliwa, aliwapongeza Wahandisi wa Mkoa wa Singida kwa ubunifu huo mpya wa ujenzi wa daraja hilo na kutaka teknolojia hiyo isambae katika mikoa yote nchini.

"Kupitia vikao vyenu vya TANROAD na TARURA hii taaluma muifikishe kwa mainjinia ili kila injinia kwenye mkoa wake atafute fursa na bahati nzuri mawe yamejaa kwenye maeneo yetu," alisema.

Majaliwa alisema serikali imekuwa ikigharamia fedha nyingi kujenga madaraja kwa gharama kubwa wakati kumbe kuna Watanzania wabunifu wenye taaluma zao wanaweza kujenga madaraja kwa gharama nafuu.

"Daraja hili hapa miaka yote tulishindwa kulijenga sababu ya gharama na ilikuwa lazima tupate zaidi ya shilingi milioni 500 kumbe mainjinia wetu na usomi wao wana uwezo wa kujenga daraja la kudumu kwa gharama nafuu," alisema.

Aidha  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa baada ya  kukagua daraja hilo alipata fursa ya kuzindua Jengo la Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mkalama lililokamilika kwa asilimia 100 ambalo limejengwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) kwa gharama ya  Sh. 1.33 Bilioni  bila ya VAT.

 Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Dk. Festo Dugange, alisema serikali imekubaliana na wahandisi wa TARURA kuendelea kuwa wabunifu na kwamba Wilaya ya Mkalama imeongezewa bajeti ya ujenzi wa barabara kutoka Sh.600 milioni hadi kufikia Sh.2.2 bilioni.

 

Post a Comment

0 Comments