Ticker

6/recent/ticker-posts

JUMLA YA WAOMBAJI 106,295 WAMETUMA MAOMBI YA KUJIUNGA KATIKA VYUO 76 NCHINI


 Katibu Mtendaji Mkuu Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), Prof.Charles Kihampa akizungumza na waandishi wa habari leo Agosti 24,2022 Jijini Dar es Salaam.

*****

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Jumla ya waombaji 106,295 wametuma maombi ya kujiunga katika Vyuo 76 vilivyoidhinishwa kudahili.

Aidha Jumla ya programu 757 zimeruhusiwa kudahili ikilinganishwa na programu 724 mwaka 2021/2022.

Ameyasema hayo leo Agosti 24,2022 Jijini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji Mkuu Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), Prof.Charles Kihampa wakati akitoa taarifa hiyo kwa Waandishi wa habari.

Amesema kwa mwaka huu kuna jumla ya nafasi 172,168 ikilinganishwa na nafasi 164,901 mwaka uliopita. Hii ni ongezeko la nafasi 7,267 sawa na asilimia 4.4 katika programu za shahada ya kwanza.

“Katika mwaka wa kwanza ya udahili, Jumla ya waombaji 75,163 sawa na asilimia 70.71 ya waombaji wote walioomba udahili wameshapata udahili vyuoni”. Amesema Prof.Kihampa.

Aidha amesema mwenendo wa udahili wa awamu ya kwanza kwa kipindi Cha miaka mitano (2018/2019 hadi 2022/2023) unaonesha ongezeko kubwa la waombaji ikiashiria ongezeko la wahitimu wa kidato cha Sita na wale wa Stashahada.

Pamoja na hayo Prof.Kihampa ametoa wito kwa waombaji udahili wa shahada ya kwanza wanakumbushwa kuwa masuala yote yanayohusu udahili au kujithibitisha katika chuo kimoja yawasikishwe moja kwa moja kwenye vyuo husika.

“Kwa wale ambao watapata changamoto katika kujithibitisha, vyuo vyote vimeelekezwa kupokea taarifa zao na kutafuta ufumbuzi wa haraka kwa kuzingatia miongozo na taratibu zilizowekwa”. Amesema

Post a Comment

0 Comments