Ticker

6/recent/ticker-posts

ASILIMIA 95 ZIMEFIKIWA UKARABATI KIWANDA CHA MPONDE, WAKULIMA WA CHAI KICHEKO.

Ofisa Mtendaji mkuu wa Kiwanda cha Mponde Temba Kassim akieleza jambo kwa Waziri Ndalichako.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu Joyce Ndalichako akiwa katika ukaguzi kwenye kiwanda cha chai Mponde, wa kwanza kulia ni mkuu wa Mkoa wa Tanga Omari Mgumba na kushoto ni mkuu wa Wilaya ya Lushoto Kalisti Lazaro.


********************

Na Hamida Kamchalla, LUSHOTO

WAKULIMA wa zao la chai katika kiwanda cha Mponde kilichopo halmashauri ya Bumbuli Wilaya ya Lushoto wamesema serikali imefanya jambo la kuwanusuru kwa kuwafufulia kiwanda hicho.

Wamesema baada ya kufungwa kiwanda hicho walikuta tamaa ya kulinda zao la chai kutokana na kukosa solo la uhakika huku wakiishukuru serikali kwa kukamilisha kiwanda hicho na kwamba sasa wana matumaini ya kuuza chai yao kiwandani hapo.

Pia wakulima hao wameiomba serikali iangalie namna ya kuongeza bei ya ununuzi wa chai ili waweze kuona faida ya kilimo chao ambapo wamelalamika bei iliyopo sasa ni ndogo.

" Sasa hivi tunauza kilo moja sh 314 hii bei ni ndogo sana hivyo, tunaiomba serikali iangalie namna ya kupandisha angalau ifike hata 700 au 1000 ili iendane na garama za uendeshaji maana sasa hivi Bei ya pembejeo sio kama ya zamani, amesema

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Joyce Nalichako akiongea na wakulima hao juzi amesema serikali imedhamiria kukifungua kiwanda cha chai Mponde kilichopo ili kuinua uchumi wa wakulima wao.

Amesema kwa sasa kiwanda hicho kimefikia asilimia 95 ya maboresho na kwamba mpaka ifikapo mwisho wa mwezi wa tisa kitakuwa kimekamilika na kitaanza kazi rasmi.

Ndalichako amesema serikali imewekeza sh bilioni 9 katika kiwanda hicho lengo likiwa ni kufanya ukarabati pamoja na masuala mengine yanayohusu kiwanda hicho.

"Serikali inadhamira ya dhati kufufua kiwanda hiki na ndio maana imetoa shilingi bilioni 9 na mpaka sasa bilioni 4 zimetumika kwa ajili ya ukarabati na hizo bilioni 5 zitawasaidia kuanzia kama mtaji" amesema Ndalichako.

Hata hivyo amebainisha kuwa serikali imejiridhisha kwamba kiwanda kipo tayari kuanza kazi mwishoni mwa mwezi wa 9 baada ya kukamilisha uwekaji wa mambomba ya kukaushia chai ambayo ameelekeza kazi hiyo iharakishwe ili kiwanda kiweze kukanza kazi kama ilivyopangwa.

Naye Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Amir Shehiza alisema kiwanda hicho kina zaidi ya miaka kumi toka kifungwe na kilikuwa kinategemewa kwa kukuza uchumi wa wananchi na pia kilikuwa chanzo cha mapato cha halmashauri ya Bumbuli.

"Kufungwa kwa kiwanda hiki kumechangia kwa kiasi kikubwa kushuka kwa mapato ya halmashauri kwa kwakuwa kilikuwa chanzo kikuu cha mapato sasa kikifunguliwa tunaimani hatutakuwa wa mwisho tena katika ukusanyaji wa mapato. Amebainisha mwenyekiti wa Halmshauri hiyo.

Kiwanda hicho kinatarajiwa kutoa ajira 70 za kudumu kitakapo anza kufanya kazi na 200 vibarua.

Post a Comment

0 Comments