Ticker

6/recent/ticker-posts

CHONGOLO ALIA NA VYANZO VYA MAJI LUSHOTO



************

Na Hamida Kamchalla, LUSHOTO.


WANANCHI wilayani Lushoto Mkoa wa Tanga wamehimizwa kutunza mazingira na vyanzo vya maji ili kuepuka kuyapoteza maji ambayo yanatoka kwenye maporomoko ya milima na kujiletea maisha ya ukame.


Chongolo akitoa wito huo jana katika Tarafa ya Soni wilayani humo alipoongea na wananchi akiwa kwenye ziara yake ya kikazi ambapo alisema maji yanapaswa kulindwa kwa hali yoyote ili yasipotee na kusababisha ukame.


"Kwenye maji sina tatizo, mimi wakati nakuja hapa miaka 14 iliyopita huo mto unaoambaa na maji hapo ulikuwa ni mto mkubwa, maji yamepungua sana kutokana na uharibifu wa mazingira na uharibifu wa vyanzo vya maji,


"Maji yakipungua yakaisha maana yake tunajitengenezea ugumu wa maisha kwa sababu maji ni uhai, tukikosa maji mazingira yetu ya maisha yanaathirika moja kwa moja, tunzeni vyanzo vya maji" alisema.


Aidha Chongolo alisema, mbali na hilo kuna suala la serikali kupanga maendeleo ambapo inahitaji kujua idadi sahihi ya wananchi wake kwani ndicho kipaumbele chake kujua idadi wa watu katika maeneo waliyopo.


"Pamoja na kuongeza mambo ya maendeleo, ili tufanikiwe serikali inatakiwe ijue tuko wangapi, isipojua hatuwezi kufanikiwa katika mambo ya maendeleo, familia ukitaka kufanya jambo lolote lile ni lazima uweke bajeti, hivyo hivyo kwa serikali, inaweka vipaumbele kwa kujua idadi ya watu kwenye eneo" alibainisha Chongolo.


Wito wangu kwenu wana Soni, mjitokezeni kuhesabiwa kwa nidhamu, sensa siyo siasa, maana yake ni unaenda kujulikana, na mtu atakayebagua mtu kutokana na itikadi au maumbile yake huyo hana maana na wala hajui umuhimu wa sensa, tengenezeni mpango mjitokeze" alisisitiza.


Akiongelea kuhusu maendeleo, mkuu wa Mkoa wa Tanga Omari Mgumba alisema serikali imewekwa mkakati wa kuinua uchumi wa Mkoa huo kupitia viwanda pamoja na Bandari ya Tanga ambayo kwa sasa inafanya vizuri kwa kuongeza shehena kwa kiasi kikubwa ikiwa bado ujenzi unaoendelea.


"Maboresho makubwa yaliyofanyika katika Bandari yetu ya kuongeza shehena yameweza kusaidia kuongeza ukusanyaji wa mapato na kufanya Mkoa wetu kushika namba moja Kitaifa" alisema Mgumba


Hata hivyo alisema kutokana na halmashauri za Bumbuli na Korogwe vijijini kufanya vibaya katika kusimamia mapato, mkakati uliopo ni kuhakikisha wanazisaidia ili ziweze kufanya vizuri kwa zilingane na halmashauri nyingine ili kufanya Mkoa uendelee kushika nafasi hiyo.


Lakini piaba aisema kuwa Mkoa una zao la kimkakati la Mkonge ambalo kwa sasa linafanya vizuri na pia kwa upande wa viwanda serikali itahakikisha kiwanda cha chai cha Mponde kilichopo katika halmashauri ya Bumbuli, wilayani Lushoto kinafufuliwa na kufanya kazi kama awali.

Post a Comment

0 Comments