Ticker

6/recent/ticker-posts

CHONGOLO ATAKA VIJANA TANGA WAPEWE KIPAUMBELE CHA AJIRA BANDARI.



******************

Na Hamida Kamchalla, TANGA.

MRADI mkubwa wa Bandari ya Tanga unatarajiwa kuleta matokeo mazuri kwa kuongeza ajira zitakazo wainua vijana na wananchi wa Mkoa wa Tanga kwa kuwapa kipaumbele lakini pia nchi nzima na kuongeza pato la Taifa.

Chongolo amebainisha hayo alipotembelea bandarini hapo ikiwa ni moja wapo ya ziara yake kutembelea na kukagua shuhuli za miradi ya maendeleo na kutoa pongezi kwa uongozi wa Mamlaka ya Bandari Mkoa wa Tanga kwa maendeleo mazuri ya ujenzi wa mradi huo.

"Mazingira ya sasa ni tofauti kabisa na wakati ule, hongereni sana kwa mkakati wa kuhakikisha utekelezaji wa mradi unakwenda kama tulivyojiwekea kwenye utaratibu wetu,

"Lakini kikubwa niseme, haitakuwa na maana mradi mkubwa unaochukua fedha nyingi za serikali kufanyika hapa halafu usioneshe matokea chanya kwa maisha ya wananchi ya Wanatanga lakini na Watanzania kwa ujumla, kwahiyo tunategemea mradi huu utaleta matokeo chanya yatakayobadilisha maisha ya Watanzania" amesema.

Amebainisha kwamba mradi huo mara utakapomalizika kazi zitaongezeka hivyo Wanatanga wapewe kipaumbele wa kwanza kupatiwa ajira na watakaokuja kutoka Mkoa mingine watapata ajira baada ya wenyeji watakaojitokeza kupata.

"Zile kazi ambazo zitahitaji kitumia nguvu hakuna haja ya kuchukua watu kutoka mbali, vijana hapa wako wengi wakipata hizo fursa uchumi wa hapa utaongezeka na kuchangamka" amesema.

Chongolo amesema, "lakini kubwa, nipongeze sana kwamba mradi huu unakwenda kubadilisha matokeo ya usafiri na usafirishaji wa kutumia maji kwenye ukanda wa bahari kuu, ambayo sisi tumepewa dhamana ya kuratibu kupitia TPA".

Kwa upande wake Kaimu Meneja wa Bandari Mkoa wa Tanga Masoud Athumani amesema bandari hiyo ujenzi wa mradi huo ulianza kutekelezwa Agosti 2, 2019 kwa kuongezwa kina kutoka mita 3 hadi 13 ambapo uligarimu kiasi cha sh bilioni 172.3 awamu ya kwanza

"Hii awamu ya pili ulianza kutekelezwa Septemba 5, 2020 ambao ulitakiwa kutekelezwa kwa muda wa miezi 22, na ulitakiwa kukamilika Octoba mwaka huu, lakini kutokana na tatizo la ugonjwa wa Uviko 19 ulisimama kidogo na sasa wameomba waongezewe siku 43, hivyo utakamilika Novemba 28 mwaka huu, na umegarimu kiasi cha sh bilioni 256.3" amebainisha.

Amefafanua kuwa ujenzi umeingia baharini mita 50 kutokea upande wa mashariki na Miata 92 upande wa magharibi na kwamba mpaka sasa umekamulika kwa asilimia 91, huku matarajio yao ya kukabidhiwa mradi Novemba 28 wa Gati mbili wenye jumla ya mita 450.

"Tutakuwa na uwezo wa kuingiza neli mbili kubwa zenye urefi wa mita 220 kwa kila moja, ambapo kila meli yenye uwezo wa kukaa kwenye kina cha mita 13 inaweza kuingia kwenye bandari hii.

"Faida tutakazopata baada ya kukamilika kwa mradi huu, kwanza ni tutaweka kuingiza meli moja kwa moja bandarini lakini cha pili turapunguza garama kwa mteja ambapo awali alikuwa analipia mara mbili sasa atalipwa mara moja na kwa kupunguza garama tutaongea wateja, sisi kwa mwaka tunahidumia tani laki 7, 18, lakini kukamilika kwa mradi tutajua tukigaramia tani milioni 3" amefafanua

Post a Comment

0 Comments