Ticker

6/recent/ticker-posts

RAIS SAMIA AFANYA ZIARA MKOA WA TANGA, KUZINDUA CHUO CHA MAFUNZO YA JESHI LA UHAMIAJI.*************

Na Hamida Kamchalla, TANGA.

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Sulluhu Hassan anatarajia kufanya ziara ya siku mbili Mkoa wa Tanga kuanzia siku ya jumali Agosti 14 na 15, ambapo atawasili majira ya saa 8 mchana.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Omari Mgumba amethibitisha hilo leo katika kikao cha watumishi na viongozi kutoka Idara mbalimbali wakiwa katika makabidhiano ya Mkoa huo.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza ambaye alikuwa mkoani Tanga amemkabidhi Omari Mgumba aliyekuwa mkuu wa Mkoa wa Songwe.

Aidha Mgumba amesema, "Lengo la ziara yake ni kwenda kufanya uzinduzi wa Chuo cha mafunzo ya Jeshi la Uhamiaji kilichopo katika kijiji cha Manza, Wilaya ya Mkinga ambapo mbali na Hilo pia atafunga mafunzo ya Jeshi hilo waliomaliza wapatao 818" amesema

Post a Comment

0 Comments