Ticker

6/recent/ticker-posts

DK.NDIEGE:WAFUJAJI WA FEDHA ZA USHIRIKA WACHUKULIWA HATUA

Mrajisi wa Vyama vya Ushirika na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Dk.Benson Ndiege akizungumza na waandishi habari kuhusiana na mafanikio na mikakati ya Tume hiyo jijini Mbeya.

****************************

NA MWANDISHI WETU

Mrajisi wa Vyama vya Ushirika na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Dkt.Benson Ndiege amesema Sekta ndogo ya Ushirika ni Sekta wezeshi katika kuwainua wananchi kiuchumi kutokana na umojaa wao kuzalisha .

Dk.Ndiege aliyasema hayo wakati akizungumza na Waandishi habari kuhusiana na mikakati ya Tume ya Maendeleo ya Ushirika Jijini Mbeya

Sekta ya ushirika inajumuisha Kilimo, Fedha, Madini, Mifugo, Viwanda na Usafirishaji. Sekta hii inasimamiwa na Tume ya Maendeleo ya Ushirika (TCDC) ambayo ni idara ya Serikali inayojitegemea iliyo chini ya Wizara ya Kilimo katika kipindi cha Julai 2021 hadi Juni 2022, idadi ya Vyama vilivyosajiliwa ilifikia 9,741 ikilinganishwa na Vyama 9,185 katika kipindi hicho cha mwaka 2021 kati ya Vyama vilivyosajiliwa, 4,538 ni Vyama vya Ushirika wa Kilimo na Masoko (AMCOS), 3,946 ni Vyama vya Ushirika wa Akiba na Mikopo (SACCOS) na 1,257 ni Vyama vinavyojishughulisha na kazi mbalimbali zikiwemo ufugaji nyuki, ufugaji, madini na uvuvi huku idadi ya wanachama wa Vyama vya ushirika imeongezeka kutoka wanachama 6,050,324 mwaka 2020/2021 kufikia wanachama 6,965,272 kwa mwaka 2021/2022.

Amesema uhamasishaji umejielekeza zaidi kwenye mazao au aeneo ambayo ambayo huko nyuma hayakupewa kipaumbele au hayakuhudumiwa na ushirika.

Amesema ukaguzi wa uyama vya Ushirika Tume katika mwaka 2021/2022, itaendelea kuimarisha ukaguzi katika Vyama vya Ushirika, ambapo kati ya Julai 2021 na Juni 2022, Vyama vya Ushirika 6,013 kati ya Vyama 9,185 vilikaguliwa. Matokeo ya ukaguzi huo ni pamoja na kubainika kuwepo kwa ukiukwaji wa taratibu za uendeshaji wa Vyama vya Ushirika, na hivyo kusababisha kutokea kwa upotevu au hasara ya fedha na mali kwa baadhi ya Vyama vya Ushirika.

Aidha amesema imebainika kuwa Vyama vya Ushirika vina mifumo mibovu ya udhibiti wa ndani pia baadhi ya vyama vinashindwa kuandika miamala ya fedha kulingana na taratibu za fedha zilizopo na hatua zilizohukuliwa pamoja kuwaondoa na wengene kuwatengua Viongozi17 wa Bodi za Vyama viwili vya Upili na wajumbe 224 wa Bodi katika Vyama vya Msingi 32 kutoka Mikoa 15 walioshindwa kusimamia vyama vyao ipasavyo.

Dk.Ndiege amesema viongozi waliobainika kuhusika na vitendo vya wizi na ubadhirifu wamefikishwa kwenye vyombo vya Dola kwa ajili ya taratibu nyingine za kisheria ikiwemo mahakama na mashauri yake yanaendelea

Aidha amesema katika kuimarisha usimamizi wa vyama vya Ushirika nchini kuwajengea uwezo maafisa Ushirika nchini na viongozi wa vyama vya ushirika ili kukabiliana na changamoto ya utendaji usioridhisha na ubadhirifu katika Vyama vya Ushirika hivyo Tume kati ya Julai 2021 na Juni 2022 imewajengea uwezo Maafisa Ushirika 170 kutoka mikoa 13 ya Mwanza, Tabora, Shinyanga, Geita, Mara, Kigoma, Kagera, Simiyu, Iringa, Njombe, Mtwara, Ruvuma na Lindi. Aidha, Viongozi 17,423 na wanachama 197,968 wa Vyama vya Ushirika walipatiwa mafunzo mbalimbali kwa lengo la kuimarisha usimamizi na uendeshaji wa vyama.

Dk.Ndiege amesema Tume ilinunua vitendea kazi katika kuimarisha utendaji kazi wa maafisa Ushirika Nchini ambavyo ni magari 12, pikipiki 137 na Kompyuta 82. Vitendea kazi hivi vimegawanywa kwa Maafisa Ushirika kote nchini.

Amesema Tume imetengeneza mfumo wa Kielektroniki wa Usimamizi na ukaguzi wa Vyama vya Ushirika na Mfumo wa Kielektroniki wa Usimamizi na Ukaguzi wa Vyama vya Ushirika na unatarajiwa kuzinduliwa mwezi Agosti, 2022 ambapo mifumo hiyo itarahisisha mkulima na mwanaushirika kupata taarifa sahihi za utendaji katika Ushirika katika maeneo ya uwekezaji, mikopo ya pembejeo na marejesho ya mkopo kwa mkulima, bei na malipo ya mazao ya mkulima.

Hata hivyo Dk.Ndiege amesema katika kuimarisha Usimamizi wa vyama vya Ushirika Tume katika mwaka wa fedha 2021/2022 imeandaa Miongozo 15 itakayotumika katika kusimamia Vyama vya Ushirika nchini na miongozo hiyo inahusu maeneo ya ufilisi, uwekezaji na usajili wa rehani, utatuzi wa migogoro, ukaguzi wa Vyama vya Ushirika visivyo vya kifedha, ukaguzi wa Vyama vya Ushirika vya kifedha, udhibiti wa majanga, uwekezaji, mawasiliano, utumishi, ununuzi kwenye Vyama vya Ushirika, uanzishaji na uendeshaji wa mifuko ya pembejeo na usimamizi wa AMCOS za miwa nchini.Tume hiyo imeendelea kutoa leseni za uendeshaji wa Vyama vya Ushirika vya Akiba na Mikopo kwa mujibu wa Sheia ya Huduma Ndogo za Fedha ya mwaka 2018. Katika mwaka 2021/2022 SACCOS 258 zimepatiwa Leseni na hivyo kufanya idadi ya SACCOS zenye leseni kufikia 691. Kati ya hizo, SACCOS daraja A ni 559 na SACCOS daraja B ni 132. Adha, hadi kufikia Juni 2022, SACCOS zilizopatiwa Leseni zilikuwa na Hisa za Shilingi 134,877,711,804 (Bilioni 134.9), Mali za Shilingi 836,748,800,326 (Bilioni 836.7), Akiba na Amana ni Shilingi 576,013,761,248 (Bilioni 576), na mikopo iliyotolewa kwa wanachama ni Shilingi 639,432,753,633 (Bilioni 639.4).

Amesema kuimarisha upatikanaji wa Pembejeo kupitia Ushirika Manufaa ya Ushirika ni pamoja na urahisi wa upatikanaji wa pembejeo kwa Vyama vya Ushirika wa mazao. Katika kipindi cha Julai 2021 hadi Juni 2022, Tume imeendelea kuratibu upatikanaji na usambazaji wa pembejeo za mazao ya pamba, tumbaku, chai, kahawa na korosho ambapo pembejeo zenye thamani ya Shilingi 178,844,086,527.4 zimenunuliwa na kusambazwa kwa wakulima kupitia AMCOS kama ifuatavyo: Mbolea Tani 34,391.80 (Shilingi 63,047,095,742.40), Mbegu Tani 21,104.24 (Shilingi 17,415,820,097.00), Viatilifu Tani 13,606.775 (Shilingi 17,770,119,000), Lita 1,452,248 (Shilingi 41,585,952,000) na Ekapacks 8,639,309 (Shilingi 38,876,890,588)), Vinyunyizi Vipande 121 (Shilingi 133,100,000) na Vifungashio Vipande 2,928,985 (Shilingi. 15,108,876,224).

Dk. Ndiege amesema mauzo ya Mazao kupitia Vyama vya Ushirika uwezeshwaji wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika kwa Vyama vya Ushirika umefanyika pia kwa kuvisimamia Vyama vya Ushirika wa Kilimo na Masoko (AMCOS) katika kukusanya na kuuza mazao ya wakulima ambapo hadi Juni, 2022 tani 588,020,627.7 za mazao yenye thamani ya Shilingi 1,669,891,702,798.5 ziliuzwa kupitia Vyama vya Ushirika kupitia Mfumo wa Stakabadhi za Ghala na minada.

Tume inahamasisha Wanawake kujiunga na ushrika ambao ni Wajasiriamali, Wafanyabiashara, Wafugaji, Wavuvi, Wasusi, Mafundi, Wakulima na wazalishaji kwenye shughuli nyingine za kiuchumi za Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu au mahitaji maalum kujiunga pamoja na kuanzisha Ushirika utakaokuwa kwa kutumia muundo wa Madirisha “Business Model”. Hii ni utekelezaji wa Mikataba na Maazimio mbalimbali ya Kikanda na Kimataifa na Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya Mwaka 2020 – 2025.

Amesema Tume imeendelea kuhamasisha Vyama Vikuu vya Ushirika kuanzisha kampuni ambapo hadi Juni 2022, Vyama Vikuu vya Karagwe District Cooperative Union – KDCU, Kahama Cooperative Union - KACU, Chato Cooperative Union – CCU na Umoja Liwale vimeanzisha kampuni kwa ajili ya biashara za mazao.Amesema Tume inatarajia kuanzisha wa Benki ya Taifa ya Ushirika ikiwa ni pamoja kuratibu uanzishwaji wa Benki ya Taifa ya Ushirika ambayo itamilikiwa na Vyama vya Ushirika kwa asilimia 51 na taasisi na watu binafsi watamiliki kwa asilimia 49 lengo la kuanzishwa Benki hiyo ni kurahisisha upatikanaji wa mitaji kwa wanachama na mtaji wake wa kuanzishwa Bilioni 15 hadi sasa benki hiyo mtaji wake umefikia Shilingi Bilioni 3.7.

Post a Comment

0 Comments