Ticker

6/recent/ticker-posts

MAONESHO YA KAZI ZA KISAYANSI KITAIFA KUFANYIKA DESEMBA 8,2022

Mwanzilishi Mwenza Shirikisho la Wanasayansi Chipukizi (YST) Dkt.Gozibert Kamugisha akizungumza na waandishi wa habari leo Agosti 14,2022 katika Hoteli ya Golden Tulip Jijini Dar es Salaam Afisa Mtendaji wa Karimjee Jivanjee Foundation Bi.Caren Rowland akizungumza na waandishi wa habari leo Agosti 14,2022 katika Hoteli ya Golden Tulip Jijini Dar es Salaam Afisa Mtendaji wa Karimjee Jivanjee Foundation Bi.Caren Rowland akizungumza na waandishi wa habari leo Agosti 14,2022 katika Hoteli ya Golden Tulip Jijini Dar es Salaam

********************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Shirikisho la Wanasayansi Chipukizi (YST) kwa mwaka huu 2022 imepokea idadi kubwa ya maombi ya kazi za kisayansi kutoka kwa wanafunzi wanaomba kushiriki mashindano ya sayansi yanayofikia 1,143 ambayo yatafanyika katika kila mkoa nchini.

Hili ni ongezeko la 92.4% kwa idadi ya kazi za kisayansi zilizowasilishwa mwaka huu ukilinganisha na mwaka jana 2021.

Ameyasema hayo leo Agosti 14,2022 Mwanzilishi Mwenza YST Dkt.Gozibert Kamugisha katika mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika kwenye hoteli ya Golden Tulip Jijini Dar es Salaam.

Amesema ongezeko hilo ni ni ishara kuwa program ya YST imepokelewa vizuri na kustawishwa katika mikoa ambapo mamlaka za mikoa zimeshiriki kikamilifu katika uendeshaji wa programu hii.

"Mwaka huu Maonesho ya Kisayansi yatafanyika katika kila mkoa nchini ambapo yamepangwa kufanyika mwezi Oktoba 2022 na zaidi ya kazi za kisayansi 336 zitaoneshwa katika mikoa mbalimbali". Amesema

Amesema kuwa Idadi ya kazi za Kisayansi zisizopungua sita zenye ubora zitachaguliwa kutoka kila maonesho ya mkoa ili zishiriki katika maonesho ya kisayansi ya kitaifa yaliyopangwa kufanyika Desemba 8,2022

Aidha Dkt.Kamugisha amesema kuwa Mwaka huu maonesho ya gunduzi na tafiti za kisayansi za kitaifa yatahusisha tafiti na gunduzi za kisayansi zisizopungua 168.

Pamoja na hayo amesema Mwaka 2021, maombi 594 ya kazi za sayansi yaliwasilishwa na wanafunzi kwa YST ambapo kazi za sayansi 204 zilikubaliwa kushiriki maonesho ngazi ya mikoa na kutoka ngazi ya mikoa kazi za sayansi 172 zilichaguliwa kushiriki maaonesho ya kisayansi kitaifa

"Kwa mwaka huo, maonesho ya kisayansi kitaifa yalifanyika katika mikoa 24 yakihusisha wanafunzi 408 na walimu 204. Na kwa mwaka huu 2022, idadi ya maombi ya kazi za kisayansi za wanafunzi wanaomba kushiriki mashindano ya kisayansi imeongezeka takribani mara mbili" . Amesema

Kwa upande wake Afisa Mtendaji wa Karimjee Jivanjee Foundation Bi.Caren Rowland amesema wamekuwa wafadhiri wa kujivunia na taasisi ya Young Scientist Tanzania (YST) kwa miaka 12 mfululizo, ikiwa ni pamoja na kutoa udhamini wa elimu ya juu kwa wanafunzi wote washindi wa YST kwa watakaosoma na kuhitimu masomo yao ya Chuo Kikuu baada ya kumaliza masomo yao ya elimu ya juu.

Amesema mpaka sasa Karimjee imeshadhamini wanafunzi 37 kufikia mwaka 2021 na itaendelea kudhamini pia wanafunzi wanne watakaoshinda mwaka huu na kufikia idadi ya wanafunzi 41 hadi mwaka 2022.

"Kwa miaka 12 Karimjee Foundation imekuwa ikitoa mkono wa uhisani kwa YST, ]kwa mwanzo hafifu YST ilianza na shule 4 hapo mnamo mwaka 2011, mpaka kufikia kuwa na maonesho ya kitaifa na sherehe za Tuzo kitaifa pia. Na wameweza kufikia shule zote za Tanzania bara na Visiwani". Ammesema Bi.Caren

Hata hivyo amesema kuwa Mwaka huu YST itakuwa inasheherekea mwaka wa 12 wa maonesho ya teknolojia na uboreshaji wa sayansi kwa wanafunzi wote nchini.Karimjee Jivanjee Foundation inafurahi kuona upanuzi huu mzuri wa mradi na kufikia shule za mikoa yote nchini Tanzania.

Post a Comment

0 Comments