Ticker

6/recent/ticker-posts

MAUAJI YA WATU WAWILI WALIOOKOTWA WAKIWA KWENYE VIROBA WILAYA YA KILINDI, WAZIRI MASAUNI ATOA NENO.

Mkuu wa Mkoa wa Tanga Omari Mgumba katikati alisisitiza jambo mbele ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Hamadi Masauni wakiwa katika kituo cha polisi Wilaya ya Kilindi kabla ya kwenda kuangalia miili ya marehemu katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali teule ya KKKT wilayani humo, wa pili kulia mkuu wa Wilaya ya Kilindi Abel Busalama.

**********************


Na Hamida Kamchalla, KILINDI

KUFUATIA tukio la watu kuokotwa kwenye viroba Wilaya ya Kilindi mkoani Tanga Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Hamadi Masauni ameelezea kusikitishwa kwake na kusema uchunguzi wa kina unaoendelea kufanyika ili kubaini waliohusika na tukio hilo.

Masauni aliyasema hayo jana wakati walipotembelea katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali teule ya KKKT wilayani humo akiwa ameambata na na kamati ya ulinzi na usalama baada ya habari ya tukio hilo kuripotiwa katika gazeti la Nipashe jana Agosti 17.

"Tumesikitishwa na tukio hili la kinyama, tumeshuhufia maiti na tumepatta maelezo kutoka kwa madaktari na vyombo vyetu vya usalama, japokuwa ni mapema mno kusema, nitoe wito kwa jeshi la polisi kuendelea kufanya uchunguzi wa kina hasa ili kubaini aliyehusika na tukio hili la kinyama dhidi ya raia wenzetu" alisema.

"Jambo hili halikubaliki kwa namna yoyote ile, siyo utamaduni Wala desturi yetu, na hata katika mazingira ambayo wametekelza matukio haya ni jambo ambalo, kama serikali tuwaeleze wananchi kwamba tutalichulia kwa uzito mkubwa na tutafanya kila linalowezekana tuhakikishe vyombo vyetu vya usalama vinawatia mikononi wahusika" alibainisha.

Aidha Masauni alibainisha kwamba jambo Hilo linaonesha Kuna uwezekano wa kuwepo kwa hali ya uhalifu aidha Kuna ujambazi au watu wanaotumia majambazi katika kutekeleza uhalifu huo na wa aina nyingine.

"Lakini kwa namna yoyote ile uchunguzi ndiyo utakaotuwezesha kujua ukweli, lakini cha umuhimu zaidi ni kuhakikisha wale waliofanya uhalifu huu wanapatikana mara moja na sheria kuchukua mkondo wake" alibainisha.

Mkuu wa Mkoa wa Tanga Omari Mgumba alisema tukio hilo limeleta taharuki katika Mkoa pamoja na nchi kwa ujumla kwani limesababisha watu kushindwa kufanya shuhuli zao na kutaka kwenda hospitali kujiridhisha kuangalia ndugu zao.

"Lakini pia tukio kama hili limeuchafua Mkoa wetu na Taifa letu kwa sababu uhalifu huu uni kama uhalifu mwengine, kwahiyo nataka niwahakikishie kwamba Tanga itaendelea kuwa salama na majeshi yetu tote ya ulinzi na usalama yatafanya jitihafa" alisema.

Hata hivyo Mgumba amefafanua kwamba kwa uchunguzi wa awali inaonesha tukio la mauaji hayo halikutekepezwa mkoani humo isipokuwa wauaji walikwenda kuitupa miili hiyo katika Wilaya hiyo.

"Kwasababu ukiangalia zile picha watu walmepakiea kwenye viroba vya kg 50 lakini wamekunjwa kama vya vya kg 20 inaonekana ni watu wazoefu wa shuhuli hii ya mauaji" amebainisha .

Marehemu hao wawili waliokotwa Agosti 11 katika kata ya Tunguli ambapo wanadhaniwa kuwa ni wauzaji wa Madini na walikuja kutupwa katika eneo hilo baada ya kuuawa na Watu wasiojulikana.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga Safia Jongo alisema, "tumepokea kwa masikitiko tukio hili lakini tulishaanza kufanya uchunguzi, lakini pia makao makuu ya polisi yameshaunda time itakayokuja kushirikiana na sisi kufanya uchunguzi wa kina ili kuwapatia wahalifu" amesisitiza Jongo.

Post a Comment

0 Comments