Ticker

6/recent/ticker-posts

KAYA KUTOKA NGORONGORO ZAENDELEA KUMIMINIKA KIJIJI CHA MSOMERA, KESHO WATU ZAIDI YA 200 WAPOKELEWA.


*********************

ZAIDI ya kaya 25 kutoka Wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha kesho zinatarajiwa kuwasili katika kijiji cha Msomera, wilayani Handeni Mkoa wa Tanga ili kuungana na wenzako ambao walishahamia.


Akiongea akiwa katika kijiji hicho leo, mkuu wa Mkoa wa Tanga Omari Mgumba amesema Mkoa uko tayari kuwapokea na kwamba wanaendelea kuimarisha miundombinu katika maeneo hayo kwa ajili ya huduma za jamii kwa ajili yao.


"Nimekuja kusalimiana na ndugu zetu wa Msomera lakini pia kukagua shuhuli za ujenzi zinavyoendelea, na tunaendelea kupokea na tunategemea kupokea ndugu zetu wa Ngorongoro ambao wanakuja kwa hiyari"


"Kesho tarehe 19 tunatarajia kupokea ugeni wa kundi la pili kutoka Ngorongoro zaidi ya kaya 25, zaidi ya wananchi 200 na mifugo zaidi ya 700, sasa niliona kabla sijapokea wageni nigije Mimi kwanza kwa sababu mimi ni mkuu wa Mkoa na sijawahi kufika hapa" amefafanua.


"Nimeridhika na kazi inavyoendelea, kwa mujibu wa mkataba kazi hizi tulikuwa tukabidhiwe Septemba 30, lakini kutokana na umahiri wa jeshi kwa kazi nzuri inayofanya na Suma JKT amesema kwamba tukamilishe 30 Agosti" amebainisha


Naye Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga Safia Jongo amefafanua kwamba wanaishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kusikiliza ombi lao la kuomba eneo kwa ajili ya kujenga kituo cha polisi katika kijiji hicho kutakana na kwamba awali eneo hilo halikuwepo kwenye ramani.


"Tunaishukuru sana Rais wetu mpendwa Samia Sulluhu Hassan kwa kusikia kilio chetu, kwa sababu hapo awali wakati nyumba hizi zinajengwa hapakuwa na ramani ya kituo cha polisi, lakini nilipopeleka ombi na ramani wakalitilia maanani na kituo cha polisi limejengwa pamoja na nyumba za polisi" amesema Jongo.


Amefafanua kwamba jeshi la polisi haliko mbali na kijiji cha Msomera na kwamba misako inafanyika lakini pia wanakaa hapo na kulala nje kuwalinda wananchi hao pamoja na mali zao.


"Kubwa ni kuhakikisha kwamba usalama wa raia na mali zao unaimarika, sisi tumeridhishwa na hatua hii ya ujenzi inavyoenda kwenye hiki kiruo, lakini askari wapo tayari, ni suala tu la kukabidhiwa kituo na nyumba na kazi za kituo zianze mara moja" amesema.

Post a Comment

0 Comments