Ticker

6/recent/ticker-posts

MAYELE ATETEMA TENA JIJINI ARUSHA, YANGA SC IKIICHAPA COASTAL UNION************************

NA EMMANUEL MBATILO

KLABU yaYanga imeendelea kutoa dozi kwenye ligi ya NBC mara baada ya hii leo kuichapa timu ya Coastal Union kwa mabao 2-0 mchezo ambao ulipigwa kwenye dimba la Shekhe Amri Abeid Jijini Arusha.

Ni Mayele tena ambaye aliingia kipindi cha pili na kupachika bao la pili kwenye mchezo huo akipoke pasi ya kichwa kutoka kwa mkongo beki kisiki mwenzake Shaban Djuma na kuzamisha moja kwa moja nyavuni.

Bao la kwanza la Yanga lilifungwa na Benard Morrison kipindi cha kwanza akipokea pasi kutoka Jesus Moloko ambaye pia aliumia kwenye mchezo huo na kulazimishwa kutoka baada ya kuchezew rafu mbaya na mlinzi wa Coasta Union

Post a Comment

0 Comments