Ticker

6/recent/ticker-posts

NHC; KUTATUA CHANGAMOTO YA MAENEO YA MAKAZI NA BIASHARA KUVUTIA WAWEKEZAJI

Mkurugenzi Mkuu NHC Nehemiah Mchechu akiwasilisha mada katika jukwaa la Wafanyabiashara Kutoka Afrika kusini nchini.


**********************

Na Magrethy Katengu

Shirika la nyumba la Taifa (NHC) limesema litahakikisha linaenda kutatua changamoto ya maeneo ya makazi na biashara kwa kuendelea kujenga zitakazopangishwa au kuuzwa kwa gharama nafuu ili kusaidia kuendana na hali ya mwananchi wa chini naye anufaike.

Akizungumza Dar es salaam Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la nyumba (NHC) Nehemia Mchechu katika kikao na chama cha wafanyabiashara wa Afrika kusini ikiwa na lengo la kuwashirikisha kufahamu fursa zilizopo ndani ya NHC ili nao wavutiwe kuja kuwekeza kwa kupangisha au kununua majengo wanayoyajenga.

"Tunakwenda kujenga nyumba aina ya magorofa nchi nzima ili kujibu matatizo ya maeneo ya biashara na makazi ya watu ambayo tutauza na kupangisha Kwa gharama nafuu kwa kufuata taratibu zilizowekwa" amesema Mchechu

Mchechu amesema NHC kuna miradi inakwenda kutekelezwa katika Viwanja vya kawe,Magomeni Mchikichini,Temeke mwisho ,Magomeni,Kinondoni kwani maeneo hayo Kwa asili yalikuwa maeneo ya Shirika hilo hivyo mara tu watakavyorejeshewa viwanja hivyo Ujenzi utaanza mara moja.

Sanjari na hayo ameendelea kusema wanaendelea kumaliza miradi ya kimkakati ambayo ilikwama kidogo hivyo tumejipanga kutembea kutangaza kwa wawekezaji wakubwa nchi jirani ambazo zina uwezo wa kuwekeza nchini Tanzania ili kusaidia pato la Taifa kukua.

"Tunaamini wawekezaji ni Muhimu sana na sisi tunatembea katika Mapito ya Royal tour Kwa kutangaza fursa na kuwaleta wawekezaji na Shirika la nyumba tuna mikakati mipya sasa hivi tumepanga kwa kushirikiana sekta binafsi "alisema Mchechu

Naye Mwenyekiti wa jukwaa la Wafanyabiashara wa Afrika kusini Manish Thakrar amesema NHC wamewaonesha fursa nyingi za kuja kuwekeza siyo kwao peke yao wanaoweza kunufaika bali na mataifa mengine .

Sanjari na hayo amesema nyumba zinazojengwa kote Duniani hujengwa kwa kutofautiana bei ya uuzaji na kupangishwa hivyo hata wananchi walio na kipato cha juu kati na chini wote watanufaika kulingana na viwango vitajavyowekwa hivyo Shirika hilo limejipanga kumuhudumia kila mtu kwa kipato chake.

Post a Comment

0 Comments