Ticker

6/recent/ticker-posts

SERIKALI YAOMBWA KUTENGA ENEO MAALUMU LITAKALOTUMIKA KWENYE MAONESHO TCCIA

Mkuu wa Mkoa Mwanza, Adam Malima akizungumza Kwa niaba ya Waziri wa Uwekezaji,Viwanda na Biashara Dk Ashat Kijaji kwenye ufunguzi wa maonyesho ya 17 ya chemba ya wafanyabiasha na wenye viwanda na kilimo(TCCIA) yanayofanyika kwenye uwanja wa Nyamagana mkoani hapa.

*********************

Na SHEILA KATIKULA,MWANZA

Serikali imeombwa kutenga eneo maalumu ambalo litakuwa likitumika kwenye maonyesho mbalimbali ya chemba ya wafanyabiashara wenye viwanda na kilimo Tanzania(TCCIA)ili waweze kutangaza bidhaa zao wa wateja wao.

Hayo yamesemwa jana na Makamu wa Rais wa TCCIA Clement Boko kwenye maonyesho ya 17 ya Afrika Mashariki yaliyoshirikisha nchi nane ambayo yameandaliwa na TCCIA yanayofanyika kwenye uwanja wa Nyamagana mkoani hapa.

Boko amesema TCCIA ipo tayari kushirikiana na Serikali ili waweze kuweka miundo mbinu rafiki kwani kufanya hivyo itasaidia maonyesho hayo kufanyiwa kwa urahisi.

"Tunaiomba Serikali itenge eneo maalumu la kufanyia maonyesho hayo kwani TCCIA tunajitaidi kuleta makundi mbalimbali ya wafanyabiasha wakulima, wenye viwanda na wafugaji ili waweze kuonyesha bidhaa zao na kuuza kwa wakati," amesema Boko.

Naye Mwenyekiti wa TCCIA Mkoa wa Mwanza, Gabriel Kenene amesema maonyesho hayo yanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwamo kukosa sera ya kuwafanya wafanyabiashara, wenye viwanda na kilimo kujiunga na chemba, na utitiri wa kodi na ugumu wa kupata vibali mipakani kwa washiriki.

Hata hivyo Kenene ameiomba Serikali kusaidia ili wawaze kupata washiriki kutoka nchi nje ambazo watashiriki kwenye maonyesho.

Kwa upande wake katibu wa TCCIA Hassan Karambi akitoa taarifa ya maonyesho hayo Amesema kuna mabanda zaidi ya 100 ya wafanyabiashara wa ndani, 55 kutoka nchi za Afrika Mashariki na wazawa 250 wameshiriki kwenye maonyesho hayo yanayotarajia kufungwa septemba 4 mwaka huu.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Adam Malima akimwakilisha Waziri wa Uwekezaji, Viwanda, Biashara Dk. Ashanti Kijaji kwenye kufungua maonesho ya 17 ya Afrika mashariki amesema amepoke malalamiko kutoka Shirikisho la Mpira wa Mguu Tanzania (TFF) juu ya matumizi ambayo siyo ya mchezo kwenye uwanja huo.

Hata hivyo amewataka wakuu wa Wilaya ya Nyamagana na Ilemela kushirikiana kwa pamoja na TCCIA kutafuta eneo la kudumu la kufanyia maonyesho hayo.

“Mwanza inatakiwa tuitangaze kama mji wa biashara na viwanda, wakuu wa wilaya hizi wakae ndani ya wiki mbili waje waniambie eneo gani tulitumie, haya maonyesho yana heshima kubwa yanatakiwa yalete watu.”amesema Malima.

Amesema utokana na changamoto mbalimbali zilizotajwa na TCCIA ikiwemo ya wafanyabiashara kutoka nje ya nchi kucheleweshwa mipakani wanapokuwa wanavusha bidhaa zao pindi wanapokuja kwenye maonesho atahakikisha anazifanyia yum Uzi changamoto hizo ili kuendeleza mahusiano mazuri na mataifa hayo.

Post a Comment

0 Comments